WANAWAKE WAMEOMBWA KUJITOKEZA KUCHANGAMKIA KAZI YA SEKTA YA UDEREVA.



 Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Mwanza

 

- Serikali yashauriwa kuajiri madereva wengi wa kike ili kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume.

- Chama cha madereva wa Serikali Tanzania champongeza mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

SERIKALI  imeshauriwa  kuendelea kuajiri  madereva wengi  wa kike nchini kutokana na utendaji kazi wao kuwa mzuri katika sekta hiyo, kama ambavyo imekuwa  ikitoa ajira kwa wanaume  huku mabinti wakiombwa kujitokeza katika kuchangamkia fursa hiyo.  

Ushauri huo umetolewa Jijini Mwanza na Chama cha kitaaluma cha madereva wa Serikali Tanzania ( CMST ) kwenye mkutano wao ambao umefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  ukiwa na lengo la kukumbushana  ili waweze kuwa na uadilifu katika utendaji wa kazi na kuimarisha chama hicho.

Chama hicho pia kimetoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Serikali kuu kwa ujumla akiwemo mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan bila kumsahau Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasimu Majaliwa kwa kuwaunganisha nchi nzima. 

 




Previous Post Next Post