WAZIRI MBARAWA ASHIRIKI ZOEZI LA MAJARIBIO YA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU.


 Na,Swalehe Magesa Misalaba Media - Mwanza

 

Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa ameshiriki zoezi la tatu la majaribio ya Meli mpya ya kisasa ya MV Mwanza Hapa kazi tu huku akimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ujenzi wake ambao kwasasa umefikia asilimia 93 kutoka awali asilimia 40.

 

Waziri Mbarawa ameyasema hayo Jijini Mwanza wakati akikagua majaribio ya meli hiyo mpya iliyojengwa katika eneo la Mwanza kusini.

 

 Mkurugenzi wa Huduma za Meli ( Mscl ) Eric Hamiss amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambazo zimeweza kukamilisha ujenzi wa Meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu,ambapo amesema meli hiyo inatajiwa kuanza kutoa huduma za usafiri mwezi Juni mwaka huu.

 

 

 Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa amesema,Meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu,ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 110 huku asilimia kubwa ya wajenzi wake wakiwa watanzania wakishirikiana na wakorea,meli hiyo ambayo itachukua abiria 1200,magari madogo 20,magari makubwa 3 na tani 400 za mizigo huku akisema meli hiyo imekidhi viwango vya kimataifa..

 

 

 

 


 

 


 

 

 

 

 

Previous Post Next Post