Mbunge
wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Tabasam Hamis amesema wilaya hiyo
inakabiliwa na upungufu wa madawati kwa baadhi ya shule ambapo baadhi ya
wanafunzi wa shule za msingi wamekuwa wakisoma wakiwa wamekaa chini
kitendo kinachopelekea kushuka hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule
hizo.
Tabasam amebaisha
hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ilunda kata
ya Ngoma wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiwa ni muendelezo wa ziara
yake ya kata kwa kata kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali na shule
ya msingi Ilunda ikibainika kuwa na changamoto ya upungufu mkubwa wa
madawati na ina zaidi ya wanafunzi elfu moja na ikiwa na madawati sitini
pekee.
" Mimi naondoka
nakwenda Bungeni nakwenda kuzungumza na Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa
Kasimu,Spika wa Bunge Tulia Ackson,Waziri wa Serikali za mitaa Mohammed
Mchengerwa na Waziri wa elimu kuona namna ya kuongeza idadi ya
walimu,Prof Adolf Mkenda pia nakwenda kuongea na Waziri wa Mailiasili
Angellah Kairuki kwa ajili ya kutupatia kibali tuna msitu wa mbao Forest
Bugindi,roho inaniuma tuna msitu hekta elfu 17 alafu watoto wetu
wanakaaa chini Mungu anionee huruma sana katika hili,"Tabasam Hamis -
Mbunge wa Jimbo la Sengerema.
"Mheshimiwa
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameanza na miundombinu ya shule za
sekondari mama amekuta wananchi wanachanga michango mpaka elfu 40 kila
kaya,mhe Rais amesema hilo hapana kwa wananchi wa Tanzania,anasema kila
jengo litakalojengwa kwenye nchi hii la Darasa linakwenda na madawati
yake, suala la madawati Rais anawaomba mvute subira, bajeti hii
inakwenda kurekebisha suala la ukosekanaji wa madawati katika shule
zetu,"Tabasam Hamis - Mbunge wa Jimbo la Sengerema