Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba amemsimika Askofu
mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la
Orthodox nchini Tanzania.
Askofu Bukombe amesimikwa jana Jumamosi Aprili 27,2024 kwenye ibada
maalum iliyofanyika katika Kanisa la Orthodox Jimbo la Shinyanga lililopo kata
ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini, serikali
vyama vya kisiasa, wadau pamoja na waamini ambapo mgeni rasmi ni naibu Waziri
ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi.
Akizungumza Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba amemkumbusha Askofu
Bukombe kuendelea kutoa huduma hiyo kwa watu wote huku akimsisitiza kutokukata tamaa.
“Kila
mtu amepewa talanta yake na mwenyezi Mungu kiongozi yoyote awe wa Dini au wa
serikali huwa ni kionmgozi wa wote na wewe uendelee kuwa kiongozi wa wote utoe
huduma sawa kwa kila mja kwa wakristo wote ujue ya kwanza wote si sawa utapata
ambao wataitikia wito wako kuna wengine ambao hawataitikia hao wote ni wako,
kuna wale ambao utawahudumia wako na hela na kuna wale ambao utawahudumia
hawana kitu chochote hao wote ni watoto wako usije kuwakatia tama wala kukataa tama
kutoa huduma ya Mungu lakini huduma yetu si ya utajili huduma hii niya kusaidia
na kuponya watu wenye shida na matatizo kwahiyo usiogope bwana wetu Yesu kristo
awe pamoja nawe”.amesema Askofu mkuu Dkt. Jamba
Akizungumza baada ya
kusimikwa kuwa Askofu wa kanisa la Orthodox nchini Tanzania, Askofu mkuu Dkt.
Francis Laulent Bukombe ameahidi kuitumikia vema nafasi hiyo ambapo amesema
ataendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na vitendo vya ukatili unaoendelea
kwa wanawake, wanaume na watoto huku akikemea na kupinga ndoa za jinsia moja.
“Pamoja
na kutimiza utume huu kanisa litaendelea kusimama na serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Rais wetu Samia Suluhu Hassan moja wapo ya
mambo ambayo kanisa hili litasimamia n ni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia
kwa wanawake, wanaume na watoto kwahiyo kanisa hili tutasimama na kutetea kwa
nguvu zetu zote kuhakikisha tunapinga ukatili kwa watoto ubakaji na ulawiti
lakini pia vipigo vya aina zote na kuhakikisha malezi bora katika familia
yanaonekana lakini pia kanisa hili linapinga na litaendelea kupinga ndoa ya
jinsia moja mapenzi ya watu wa jinsia moja katika kanisa hili hatutafungisha
ndoa ya jinsia moja”.amesema Askofu mkuu Bukombe
Askofu Bukombe ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi
mbalimbali, wadau na waumini waliohudhulia ibada hiyo ambapo ameeleza kwa ufupi
historia katika safari yake ya utumishi pamoja na changamoto alizopitia katika
maisha yake.
“Mwaka
2003 tulianza huduma kama kituo cha huduma ya maombi na maombezi huduma hii
ilifanyika sehemu mbalimbali ambapo kwa mara ya kwanza ni nyumbani kwa Baba Deo
Majengo mapya (Diwani Mhe. Shagihilu) na badae uwanja wa Sabasaba chini ya mti
Ndala, kupitia huduma hii Mungu alinipa uwezo mkubwa wa kuwahudumia watu
miujiza ya uponyaji ilifanyika tulirudisha vitu vya watu vilivyochukuliwa na
vilivyoibiwa na mwovu mfano waliofukuzwa kazi, waliorudishwa kazini, waliokuwa
na kesi Mahakamani wengi walifutiwa na wengine kushinda kesi”.
“Muujiza mkubwa ambao utaendelea kukumbukwa ni
watu wengi kwa utukufu wa Mungu ni ule uliofanyika uwanja wa Sabasaba Mwaka
2004 ambapo mtumishi wa Mungu niliweze kuita Mvua ikakata kunyesha pia niliweza
kusimamisha Jua likatii katikati ya mkutano kwa jina la Mungu Baba kupitia Yesu
kristo mwanaye”.
“Huduma
hii haikuishia hapo tarehe 28,12,2012 huduma ya kinabii Elia Kizazi cha nne (4)
ilishuka kwa maono makubwa na nguvu ya Mungu itendayo kazi ilionekana kwa Macho
na watu kubarikiwa, kuponywa, kurejeshwa kwa upya na wengine kupokea huduma za
kinabii na mpaka leo wanamtumikia Mungu wakiwa ni manabii kwa msaada wa Mungu
tukajenga kituo cha maombi kwa kutumia Maturubai na kazi ya Mungu kuendelea
ambapo tulipata waumini wengi waliopokea baraka za Mungu Baba hadi leo hii ndani ya Mkoa wa Shinyanga nan je ya Mkoa
wetu na hata mataifa ya nje hivyo huduma hii kujulikana kimataifa” amesema
Askofu mkuu Dkt. Bukombe.
“Kwa
msaada wa Mungu tulijenga kanisa dogo na tukaanza huduma ya Orthodox mpaka
kufikia sasa tunakanisa hili ambalo leo tumefanyia ibada hii yote ni juhudi za
wakristo, wadau wa kanisa walio nje ya kanisa letu (Marafiki)amesema
Askofu mkuu Dkt. Bukombe.
“Mwaka
2015 Baba Askofu Gregoly wa Jerusaremu na Askofu mkuu wa Alexandra wa Misri
walitumwa na Patriaka wa Jerusalemu na Patrika wa Alexandra wa Misri kuniomba
kuingia na kuongoza kanisa la Orthodox ili kuliimarisha katika nchi za Afrika
Mashariki hasa Tanzania”.
“Kutokana
na kujua wito wangu katika huduma hii na mimi kwa msaada wa Mungu Baba
nilizungumza naye sirini pa sirini pake na kunipa kibali na maelekezo ya
kutumika katika utumishi huu kwa Mungu na utakatifu wake ndipo nililipoti na
kukubali wito huu nilioiyiwa”.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu
mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania Dkt. Francis Laurent Bukombe
(Bludah) akizungumza katika ibada hiyo ambapo amewashukuru viongozi, wadau na
waamini waliohudhuliwa.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu
mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania Dkt. Francis Laurent Bukombe
(Bludah) akizungumza katika ibada hiyo ambapo amewashukuru viongozi, wadau na
waamini waliohudhuliwa.
Ibada maalum ya kusimikwa uaskofu Baba Askofu mteule Francis
Laurent Bukombe (Bludah) katika kanisa takatifu katoliki la Oxthodox Tanzania
ikiendelea Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akimsimika Askofu
mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la
Orthodox nchini Tanzania.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akizungumza katika ibada hiyo.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akiwa katika zoezi la kumsimika Askofu
mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la
Orthodox nchini Tanzania.
Askofu mkuu wa Kanisa takatifu katoliki la ORTHODOX, Dkt. George Odhiambo Jamba akiwa katika zoezi la kumsimika Askofu mkuu mteule Francis Laurent Bukombe (Bludah) kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Orthodox nchini Tanzania.
Mgeni rasmi naibu Waziri
ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza katika
ibada hiyo.
Mgeni rasmi naibu Waziri
ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni mbunge
wa jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza katika
ibada hiyo.
Ibada maalum ya kusimikwa uaskofu Baba Askofu mteule Francis
Laurent Bukombe (Bludah) katika kanisa takatifu katoliki la Oxthodox Tanzania
ikiendelea Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Ibada maalum ya kusimikwa uaskofu Baba Askofu mteule Francis
Laurent Bukombe (Bludah) katika kanisa takatifu katoliki la Oxthodox Tanzania
ikiendelea Ndala Manispaa ya Shinyanga.