Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Dkt.Yudas Ndungile akizungumza leo Aprili 19,2024 kwenye kikao cha kamati
ya afya ya msingi.
Mratibu wa chanjo Mkoa wa Shinyanga Dkt. Timoth Sosoma akizungumza leo Aprili 19,2024 kwenye kikao cha kamati ya afya ya msingi.
Na Mapuli Kitina
Misalaba
SEREKALI kupitia wizaya
ya Afya Mkoani Shinyanga inatarajia kufanya kampeni ya kutoa dozi moja ya chanjo ya kuzuia saratani
ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14 baada ya tafiti
za kisanyansi kuonyesha dozi hiyo inatengeneza kinga ya kutosha
dhidi ya rika hilo.
Hayo yamebainishwa na
mratibu wa chanjo Mkoa wa Shinyanga Dkt. Timoth Sosoma baada ya kikao cha kamati
ya huduma ya afya ya msingi ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Amewasisitiza wazazi na
walezi Mkoani Shinyanga kuwapeleka watoto wenye umri huo ili waweze kupata
chanjo ikiwa lengo ni kupunguza madhara yanayoweze kujitokeza kwa vizazi
vijavyo.
Amesema kampeni ya chanjo hiyo itafanyika kwa wiki
moja ambapo itaanza Aprili 22 hadi 28 Mwaka huu 2024 na kwamba itafanyika
kwenye shule zote za msingi na sekondari (shule za serikali na binafsi) pamoja
na kwenye vituo vyote vya Afya.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,
amewaagiza viongozi wa
Serikali wakiwamo Watendaji wa Kata,na Vijiji kuwabaini wasichana ambao hawapo
mashuleni ili waweze kupata Chanjo hiyo.
DC Mkude pia amewataka
walimu kutoa ushirikiano kwa wataalam na waratibu wa kampeni hiyo katika
kuwabaini wasichana shuleni ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ambapo Mkoa wa
Shinyanga wasichana 198,865 wenye umri wa Miaka 9 hadi 14 wanatarajiwa kupata
chanjo hiyo.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt.Yudas Ndungile, amesema utoaji wa Chanjo hiyo ulianza
kutolewa Mwaka 2014 ikitolewa kwa dozi mbili, lakini kutokana na mabadiliko itatolewa
kwa dozi Moja.
Tafiti hizo
zilifanywa na shirika la Afya duniani na kudhibitishwa na kamati ya
taifa ya ushauri wa masuala ya chanjo nchini mwaka 2014 katika nchi
mbali mbali ikiwemo Tanzania.
Mkuu
wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga leo Aprili 19,2024 kwenye kikao cha kamati ya afya
ya msingi.
Kikao cha kamati ya
afya ya msingi kikiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
leo Aprili 19,2024
Kikao cha kamati ya afya ya msingi kikiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 19,2024
Kikao cha kamati ya afya ya msingi kikiendelea katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 19,2024
Picha ya pamoja baada ya kikao.