Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema
serikali Mkoani Shinyanga inatambua na kuthamini mchango wao hasa katika sekta
ya Elimu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza kwa niaba ya mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga kwenye hafla ya SHINYANGA TEACHERS NIGHT (Usiku wa Walimu)
iliyofanyika mjini Shinyanga.
DC Mhita ametumia nafasi hiyo kuwapongeza walimu
pamoja na waratibu wa hafla hiyo kwa ubunifu wao kuwakutanisha walimu huku
akisema serikali inathamini mchango wa walimu kupitia sekta ya elimu kwa
kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kusingatia misingi na maelekezo
yanayotolewa na serikali.
“Niwapongeza
sana walimu ambao mmetoka kwenye Halmashauri tatu, Halmashauri ya Manispaa ya
Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu pamoja na Halmshauri ya SHY DC kwa
kujitokeza kwa wingi kuja kushiriki usiku wa Walimu”.
“Tunathamini
sana kazi kubwa ambayo Walimu mnaifanya inawezekana hili halisemwi mara kwa
mara lakini mjue mchango wenu ni mkubwa na tunautambua mnafanya kazi kwa weledi
kusaidia jamii”.amesema DC Mhita
Mwenyekiti wa kamati ya maadalizi ya Shinyanga Teachers Night ambaye ni
Mkurugenzi wa The BSL Investiment Company Limited na BSL Schools Tanzania Mwl. Franck Peter jina maarufu MR. BLACK ametaja malengo ya hafla hiyo ikiwemo fursa
kwa walimu wote wajasiliamali na wafanyabiashara.
“Kwa
niaba ya kamati ya maandalizi ya SHINYANGA TEACHERS' NIGHT naomba kuwapa
taarifa na kuwakalibisha rasmi katika usiku uliotukuka wenye hadhi na thamani
kwa mwalimu”.
“Kwa
nini usiku wa Walimu event hii ni yenye hadhi kwa Mwalimu na imebeba maudhui
makubwa katika taaluma, uchumi na jamii. Malengo makuu ni kukutana walimu wa
kada zote yaani awali, msingi, sekondari, ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu hii
ni kuendeleza mahusiano chanya na kufahamiana zaidi”.
amesema Mr. Black
“Lakini
pia kumpa fursa Mwalimu kuonyesha bidhaa na huduma za kijasiriamali au biashara
kupitia meza za maonyesho siku ya event hii pamoja na fursa kwa walimu wote
wajasiriamali na wafanyabiashara”.
“Utoaji
wa tuzo maalumu na zawadi mbalimbali kwa walimu, kupitia mwalimu yeye mwenyewe,
shule yake au idara yake atokayo pia kupata kwa pamoja chakula, vinywaji na
burudani za hadhi yetu hakika huu ni mtoko wakiualimu na vibe kubwa ndani yake”.
“Event
hii itakua na wanenaji au waseminishaji ambao watatoa mada zenye kumgusa Mwalimu
kiuwekezaji na fursa mtandao ili kuongeza kipato cha ziada na zaidi kwa Mwalimu
pamoja na kuendeleza umoja na mshikamano baina yetu kwa kutambuana kupitia
event hizi huku tukiwa tumependeza na furaha tele”.amesema
Mr. Black
“Event hii inaandaliwa vyema kabisa na taasisi yenye
uzoefu mkubwa wa uandaaji wa matukio mbalimbali Tanzania na Africa kiujumla
yaani THE BSL INVESTMENT COMPANY LTD na THE TRUE LIFE FOUNDATION chini ya Mkurugenzi
Mwl. Peter Frank (alimaarufu MR. BLACK) ikishirikiana vyema na kamati kutoka kwa baadhi ya walimu na maafisa wa Mkoa
wa Shinyanga”
“Chakula, vinywaji na viburudisho vyote vya kisasa
kabisa vyenye hadhi ya mwalimu na pia vitaridhisha makundi yote (Mocktail na
Cocktail)”
“ Ukumbi wa kisasa kabisa MAKINDO HALL ghorofa
ya tatu ukumbi mpya wenye huduma bora na nadhifu pia utapewa access ya Wi-fi
bure njoo na simu yako tu bundle utalikuta ukumbini”.