Dr. MNZAVA, MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA SHINYANGA AADHIMISHA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KWA KUTOA VIFAA VYA MICHEZO LUBAGA SECONDARY MANISPAA YA SHINYANGA



Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga mhe. Dr. Christina  Mnzava ameadhimisha sikukuu  ya muungano  kwa kutoa VIFAA VYA michezo ambavyo vi mpira wa miguu na mpira wa netball pamoja na jezi nzuri za kisasa za netball na football. 

Dr. Mnzava akizungumza na qanafunzi na walimu wa shule ya sekondari LUBAGA iliyoko manispaa ya Shinyanga alisema
"Yeye amekuja kutimiza ahadi aliyoitoa tarehe 9.3.2024 ya kuisaidia shule vifaa vya michezo kwani vijana mnapaswa kujituma katika michezo kwasababu michezo ni Afya na michezo ni Ajira".

Ikumbukwe kuwa tarehe 9.3.2024. Mhe. Mnzava allitembelea shule ya sekondari LUBAGA na kuwapatia watoto wa kike taulo za kike za kutosha. Pia alitumia siku hiyo kuwazawadia wanafunzi wote wa kidato cha pili waliopata division one katika mtihani wao wa  mwisho wa mwaka desemba 2023 , vifaa alivyowapatia ni pamoja na daftari counter book 7 na kalamu 10 kwa  kila mtoto aliyepata daraja la kwanza. Aliwasisitiza wanafunzi wasome kwa bidii kwani yeye ataendelea kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri. 
Pia katika ziara hiyo aliahidi kuipatia shule zawadi wa photocopy ili ijiimarishe kitaaluma kwa kufanya mitihani ya kutosha ili kuinua taaluma

Naye mkuu wa shule ya sekondari LUBAGA Madame HAMISA BONIPHACE  kwa niaba ya shule alimpongeza na kumshukuru mhe. Mbunge huyo  kwa kufika shuleni hapo na kutatua changamoto ya vifaa vya michezo, taulo za kike pamoja na zawadi za kitaaluma kwa watoto waliofanya vizuri katika mitihani


Naye mwalimu wa michezo madam MULEBA LUSATO alitoa neno la shukurani kwa mhe. Mbunge kwa kuwapatia zawadi hizo za michezo na alimuahidi Mbunge huyo kuwa shule itaenda kufanya vizuri kwenye mashindano na kufika kitaifa. Pia alimtakia afya njema na mungu aendelee kumtunza. 

Nao wanafunzi viongozi wa michezo. Ndg Godfrey Maige kapteni wa mpira wa miguu na Rehema Hussein kapten wa Netball walimshukuru Mhe. Mnzava  kwa moyo wake  wa kupenda kusaidia jamii hasa wanafunzi kwa kuwapatia mipira na jezi nzuri za kisasa, na walimuahidi kuwa watacheza kwa kujituma na kufika kitaifa.



















































































Previous Post Next Post