Na Elisha Petro
Mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika Al Ahly wamefanikiwa kuitamatisha safari ya TP Mazembe kwa jumla ya magoli 3-0 baada ya ushindi wa goli 3-0 wakiwa nyumbani na kufanikiwa kutinga hatua ya fainali mbapo watamenyana dhidi ya Esperance (Tunisia) waliotinga fainali kwa kuitamatisha safari ya Mamelodi Sundown kwa jumla ya magoli (2-0) kufuatia ushindi wa goli 1-0 wakiwa ugenini sawa na ulivyokuwa nyumbani.
Kuelekea kwenye mchezo wa fainali klabu ya Al Ahly imefanikiwa kushinda michezo nane (8) katika michezo yao 15 ya mwisho waliyokutana na Esperance wao wakishinda michezo mitatu (3) pekee na wametoka sare michezo minne (4).
Jumla ya goli 19 alizofunga Al Ahly dhidi ya Esperance kwenye michezo 15 ya mwisho huku Esperance wao wakifunga goli 13 kwenye michezo waliyokutana utofauti wa magoli 2 tu katika michezo 15 waliyocheza.
Msimu jana 2012/2023 timu hizi zilikutana hatua ya nusu fainali lakini Al Ahly alifanikiwa kuwang'oa Esperance kwa jumla ya goli 4-0 baada ya ushindi wa 3-0 akiwa ugenini na 1-0 akiwa nyumbani.
Kwa ujumla tutegee kuona mechi ngumu yenye kasi nzito na matokeo yanayoweza mazito.