GILITU AFUNGA MASHINDANO YA UMISETA KANDA YA MWASELE KWA KISHINDO, AMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI


Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Lubaga ndugu Gilitu Makula leo tarehe 24.04.2024 amehitimisha mashindano ya umiseta kanda ya Mwasele yenye shule za sekondari nne ambazo ni Lubaga, Mwasele, Mwangulumbi na Hope Extended katika shule ya Sekondari Lubaga. 

Akizungumza na walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa shule zote nne, mwenyekiti Gilitu amewasihi walimu kudumisha na kuendeleza michezo maana michezo ni afya, ni ajira na michezo hudumisha mahusiano. 

Aidha, Mwenyekiti Gilitu katika kufunga mashindano hayo, Amewapatia chakula walimu, wanafunzi, na wageni zaidi ya watu 2000
Pia ametoa zawadi za fedha taslimu  sh 500,000/ kwa washindi wote ambao ni wachezaji Bora, wafungaji Bora, wanariadha walioshinda mbio zote

Pia amewazawadia MWASELE SEKONDARI mipira 3 kwakuwa ni shule iliyoshinda mpira wa miguu wavulana na netball
Aidha amewazawadia mipira 3  MWANGULUMBI SEKONDARI kwa kushinda mpira wa miguu wasichana. 

Aidha wakuu wa shule wa LUBAGA, MWASELE, HOPE NA MWANGULUMBI walimzawadia mhe.  GILITU picha kubwa yenye maneno ya shukrani. 

Naye Mkuu wa Shule ya Lubaga Madam Hamisa Boniphace kwa niaba ya wakuu wa shule wa kanda ya Mwasele alimshukuru Mwenyekiti Gilitu kwa kuwa na moyo wa kujitoa kwa jamii hasa katika sekta ya elimu na michezo

"Ndugu mgeni rasmi na mwenyekiti wetu Bodi ya shule ya Lubaga, tunakupongeza kwa dhati kwa namna ambayo umekuwa ukijitoa. Ikimbukwe na wewe mwenyewe ulituwezesha magori ya mpira wa miguu na wavu, magori na wavu wa volleyball pamoja na magoli ya mchezo wa pete. Pia tunakushukuru kwa kutupatia jezi za kutosha na mipira mitano. Na hii imekuwa ndiyo sababu ya shule yetu ya Lubaga kuchaguliwa kuwa kitu cha michezo katika kanda yetu hii ya Mwasele. Hivyo  Mwenyekiti tunakushukuru sana tena sana kwa kujitoa kwako

Naye mwakilishi wa Afisa elimu  Mwalimu CHIBUGU MUGINI  alimshukuru mhe. GILITU kwa niaba ya MKURUGENZI kwa kuwa chachu ya michezo na taaluma, alimshukuru kwa kulisha watu na kutoa zawadi tele

Michezo ya umiseta imefungwa leo hii katika ngazi za kanda.



































































































































Previous Post Next Post