BI. GIMBI MASABA ARUDISHA FOMU KUOMBA KUGOMBEA RASMI NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA KANDA YA SERENGETI

Aliyekuwa akikaimu  nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti kwa Vipindi Viwili, Bi. Gimbi Dotto Massaba Masaba tayari amerudisha Fomu ya kuomba kugombea rasmi nafasi hiyo ya Uenyekiti wa CHADEMA Kanda Serengeti.

Bi. Gimbi amerudia fomu hiyo leo Jumatatu Aprili 22,2024 ambapo amesema ni wakati wake sasa wa kuwa rasmi Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, ambayo inahudumu Mikoa Mitatu ya Simiyu, Mara na Shinyanga,

Amesema kutokana  na uwezo wake ameamua kuomba kugombea nafasi ya Uenyekiti CHADEMA kanda ya Serengeti kwa kuwa tayari anauzoefu mkubwa ambapo ameahidi kuendelea kukitumikia chama kwa kuzingatia katiba ya chama na taratibu zake.

Amesema yapo mambo mbalimbali ameyafanya wakati akikaimu nafasi hiyo na kwamba amewashukuru viongozi mbambali na wanachama wa CHADEMA kwa ushirikiano wao ambapo amesema baada ya chama chake kumpitisha katika nafasi hiyo ataendelea kufanya mambo mengi mazuri ikiwa lengo ni kuimarisha zaidi  CHADEMA.

Kwa mujibu wa kaimu katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti Bwana William Shayo, waliorudisha fomu kwa nafasi ya mwenyekiti wa kanda ya Serengeti ni watatu akiwemo Bi. Gimbi Dotto Massaba.

Zoezi la kurudisha fomu za kuomba kugombea nafasi mbalimbali CHADEMA kanda ya Serengeti  limehitimishwa leo Jumatatu Aprili 22,2024.

 

 

Aliyekuwa akikaimu  nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti kwa Vipindi Viwili, Bi. Gimbi Dotto Massaba akikabidhi fomu yake kwa kaimu katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti Bwana William Shay oleo Aprili 22,2024.





 

Previous Post Next Post