Mgeni rasmi, Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga
Bwana Joseph Taban akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza
Vihenge ambayo yameratibiwa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia mradi wa
kuthibiti Sumukuvu wa ‘Tanzania
initiative for preventing aflatoxin contamination’ (TANIPAC) ambao upo chini ya
Wizara ya Kilimo.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa
Shinyanga leo Ijumaa Aprili 26,2024 limefunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge ambapo
jumla ya vijana 58 kutoka mikoa mbalimbali wakiwemo wa Shinyanga, Geita,
Mwanza, Simiyu na Tabora wamenufaika na mafunzo hayo.
Mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayo ni
kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa shinyanga Bwana Joseph Taban ambaye amewapongeza
vijana kwa kuhitimu mafunzo huku
akiwataka kuwa mabalozi wazuri katika jamii kwa kuhakikisha wanatumia ujuzi na
maarifa waliyoyapata kuleta matokeo chanya katika jamii.
Mafunzo hayo yalianza Februari 26, 2024 kwa kundi la
kwanza washiriki walikuwa 19, kundi la pili washiriki walikuwa 23 na kundi la
tatu washiriki walikuwa 16 na kwamba yamefikia kilele leo Aprili26,2024 ikiwa
jumla ya wahitimu 58 ambao wamehitimu na kuchukua vyeti vyao.
Bwana Taban amewasihi wahitimu hao kuendeleza umoja
na ushirikiano katika kufanikisha ndoto zao kupitia ujuzi wa kutengeneza
Vihenge ili kuinuka kiuchumi.
“Ni
matumaini yangu kuwa mmepata dozi nzuri ya taaluma na mbinu mbalimbali za
kutengeneza Vihenge, mmefundishwa masuala ya ujasiliamali, utengenezaji wa
Vihenge kwa nadharia na vitendo, nadharia ya masoko, usimamizi wa fedha na
urathimishaji wa biashara”.
“Ni
matumaini yangu kuwa mafunzo mliyoyapata mtayatumia kwa vitendo kuhakikisha
kuwa lengo la mafunzo haya linatimia, pia natarajia kuwa mafunzo haya
yatawawezesha kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, kaya na taifa kwa ujumla”.
“Mafunzo
haya yametolewa kwa vijana wachache lakini wengi wangependa kupata mafunzo haya
hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba mkawe waalimu wa kufundisha vijana wenzenu
kwenye maeneo yenu ya kazi ili kwa pamoja tuweze kupambana kwa vitendo
kupunguza kama siyo kuondoa kabisa Sumukuvu”.
“Nitumie
nafasi hii kuwapongeza kwa kuwa miongoni mwa vijana wachache waliopata bahati
ya kupata mafunzo haya”.
Baadhi ya vijana ambao wamepata mafunzo hayo
wamelishukuru na kulipongeza shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa
Shinyanga kwa kutoa mafunzo hayo na kwamba wamesema yatawasaidia kwa kiasi
kikuwa kuboresha utendaji wa kazi na kuzalisha bidhaa za Vihenge (Silos) na
nyinginezo kwa tija ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya taifa la
Tanzania.
Akisoma risala ambayo imeandaliwa na wahitimu wa
mafunzo ya mradi wa kuthibiti Sumukuvu nchini kutoka kituo cha SIDO Mkoa wa
Shinyanga Wanjala Daud amesema kwenye mafunzo hayo wamejifunza kwa nadharia na
mada mbalimbali ikiwemo ujasiliamali, utengenezaji wa Vihenge kwa vitendo
(Silos), nadharia ya masoko na huduma kwa wateja, usimamizi wa fedha pamoja na
urasimishaji wa biashara.
“Tunapenda
kushukuru uongozi wa SIDO na Wizara ya Kilimo kwa kutoa fursa ya mafunzo haya
hakika yametujengea uwezo wa kujiamini na kuamsha ari ndani yetu ya kujiajiri
na kuachana na kasumba ya kusubiri ajira”.
“Pamoja
na ari na molari ya kujiajiri iliyojengeka ndani yetu tunakabiliwa na
changamoto ya mitaji kwa ajili ya kununua vifaa au vitendea kazi vya kuanzisha
shughuli mbalimbali kutoka na fani tulizojifunza hivyo tunaomba serikali
ituangalie kwa jicho la kipekee ili tuweze kujikwamua na changamoto hii na
hatimaye tuweze kujiajiri wenyewe hivyo kuchangia uchumi wetu na jamii huku
tukitokomeza kabisa Sumukuvu kwa taifa letu hili la Tanzania”.
SIDO Mkoa wa Shinyanga imetekeleza mradi wa kuzuia
Sumukuvu wa ‘Tanzania initiative for preventing aflatoxin contamination’
(TANIPAC) ambao upo chini ya Wizara ya Kilimo na kwamba mradi huo umelenga
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuimarisha usalama wa chakula na
kuimarisha Afya ya jamii.
Mradi wa TANIPAC pia umelenga kuwezesha jamii
kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususan Mahindi kutokana
na Sumukuvu.
Serikali imeingia gharama kuhakikisha kuwa vijana
wanapatiwa ujuzi wa kutengeneza vifaa vya kisasa na vinavyo dumu kwa muda mrefu
(Vihenge) ili kutimiza adhima ya kupunguza Sumukuvu.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Bwana Joseph
Taban akiwa katika zoezi la kukagua Vihenge vilivyotengenezwa na vijana ambao
wamehitimu mafunzo ya kutengeneza Vihenge kupitia mradi wa kuthibiti Sumukuvu wa ‘Tanzania initiative for preventing
aflatoxin contamination’ (TANIPAC) ambao upo chini ya Wizara ya Kilimo.

Taban na viongozi wa SIDO Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu
wa mafunzo ya mradi wa kuthibiti Sumukuvu nchini kutoka kituo cha SIDO Mkoa wa
Shinyanga leo Aprili 26,2024.

Mratibu wa Mafunzo SIDO Mkoa wa Shinyanga,
Mhandisi Manyama Lububi akizungumza
wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge leo Aprili 26,2024
Mratibu wa Mafunzo ya Kutengeneza
Vihenge Mkoa wa Shinyanga, Misuka Makwaya ambaye pia ni Mhasibu wa SIDO Mkoa wa
Shinyanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
leo Aprili 26,2024.
Afisa Mipango SIDO Shinyanga ,
Frank Nguyu akiwa katika hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge
leo Aprili 26,2024.
Wanjala Daud akisoma risala iliyoandaliwa na
wahitimu wa mafunzo ya mradi wa kuthibiti Sumukuvu nchini kutoka kituo cha SIDO
Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Bwana Joseph
Taban akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge leo
Aprili 26,2024.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Bwana Joseph
Taban akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza Vihenge leo
Aprili 26,2024.
Mgeni rasmi, Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga
Bwana Joseph Taban akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya kutengeneza
Vihenge ambayo yameratibiwa na SIDO Mkoa wa Shinyanga kupitia mradi wa
kuthibiti Sumukuvu wa ‘Tanzania
initiative for preventing aflatoxin contamination’ (TANIPAC) ambao upo chini ya
Wizara ya Kilimo.
Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga Bwana Joseph
Taban akimkabidhi cheti mhitimu wa mafunzo ya mradi wa kuthibiti Sumukuvu
nchini kutoka kituo cha SIDO Mkoa wa Shinyanga leo Aprili 26,2024.

Taban na viongozi wa SIDO wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo
ya mradi wa kuthibiti Sumukuvu nchini kutoka kituo cha SIDO Mkoa wa Shinyanga