Kueleke maadhimisho ya miaka 25 ya shirika la Compassion tangu
kuingia nchini Tanzania vituo vya maendeleo ya mtoto na kijana cluster ya Shinyanga kwa
kushirikiana na Compassion International Tanzania wameendesha zoezi la
kuchangia damu salama katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza
pamoja na kupanda miti zaidi ya 100 ili kutunza mazingira.
Mratibu wa kituo cha maendeleo ya
mtoto na kijana kanisa la EAGT ndala Bwn. Steven Simon amebainisha kuwa lengo
la kuchangia damu ni kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa kuongezewa damu.
‘‘zoezi la
kuchangia damu ni hiari sio lazima lakini tunapaswa kuguswa kila mmoja wetu
ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga kuchangia damu kwenye hospitali zetu kwani lengo kubwa ni kunusuru na kuokoa
maisha ya watu wanaopata changamoto na kuhitaji ya kuongezewa damu akiwemo mama
na mtoto’’
Kwa upande wao baadhi ya wachungaji waliohudhuria
maadhimisho hayo wamewasihi wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla
kuwa na nia moja ya kuendele kupanda na kutunza miti ili kuyalinda mazingira na
kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.
‘‘sisi kama
kanisa mazingira ni namba moja,hivyo mwanadamu yeyote aliyetimamu bila kujali
dini wala dhehebu anapaswa kuyalinda na kuyatunza mazingira kuanzia kwenye
makao yake mweneyewe na hata ndani ya jamii tunaowajibu wa kila mmoja wetu
,kila kaya,kila taasisi kuyatunza mazingira kwa kufanya usafi na kuendelea
kupanda miti ili tuepukane na mabadiliko ya tabia nchi….’’ amesema Mch. Christian Kubena
Kwa upande wake mchungaji wa kanisani
la EAGT Ndala mchungaji Andrea Salu amewasisitiza wananchi kutekeleza sera ya
nchi kwa kupanda miti mingi ili kuyafanya
mazingira kuwa rafiki zaidi kwa afya ya kila kiumbe.
‘‘…suala la kupanda miti ni ajenda ya
kitaifa ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuitekeleza kwa sababu panapotokea
ukame miti inatusaidia kuuondoa ukame huo kwa hiyo tunapaswa kuzingatia hilo
ili kuyaweka mazingira yetu kuwa mazuri nawaomba wakazi wa Shinyanga tuendelee
kushirikiana kuyaboresha mazingira yetu’’ -mchungaji
Andrea Salu.
Maadhimisho ya miaka 25 ya shirika la
Compassion tangu kuingia nchini Tanzania kitaifa yatafanyika tarehe 27.04.2024
Mkoani Tabora ambapo yatahudhuliwa na viongozi kutoka makao makuu ya Compassion
jijini Arusha,viongozi na wadau
mbalimbali.
-