Na:Elias Gamaya Ukelewe.
Ligi ya UMITASHUMTA ngazi ya Tarafa kwa mpira wa miguu, imeendelea kulindima Aprili 24, 2024 katika tarafa ya Mumbuga ili kuunda timu mahiri itakayo kwenda kushindanishwa na timu kutoka tarafa nyingine kuunda timu ya Wilaya ya Ukerewe.
Mchezo huu ulizikutanisha timu za mpira wa Miguu na Pete kutoka kata ya Nakatunguru na Bukanda, michezo ambayo imefanyika katika viwanja viwili tofauti ukiwepo Uwanja wa Getrude Mongella ambapo miamba Kakerege vs Ngoma walikutana na Uwanja wa Shule ya Msingi Kakerege nao ulikuzikutanisha timu ya kata ya Nakatunguru vs Bukanda.
Waamuzi wa katika mipambano hiyo walikuwa ni Mwl. Elybarick Denna kutoka Shule ya Msingi Mwitongo ambaye alisimamia mchezo dhidi ya Nakatunguru vs Bukanda na Walter Njuu kutoka Shule ya Msingi Malegea ambaye alisimamia mchezo dhidi ya Kakerege vs Ngoma.
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa timu kutoka kata ya Bukanda iliiadhibu timu ya Nakatunguru kwa magori 3 - 1, wafungaji wa mchezo huo ni pamoja na Baraka E. John,
Vikesi Mzobi na Edwin Lweganwa kutoka Bukanda na mchezaji Baraka Junior aliandikia timu ya kata ya Nakatunguru bao moja la kufutia machozi
Aidha, katika mchezo wa mpira wa miguu ulizikutanisha timu kutoka kata ya Kakerege vs Ngoma, watoto wa mjini Kakerege wameangukia pua kwa kunyukwa magori 2 kwa 0 dhidi ya Ngoma.
Katika mchezo wa mpira wa Pete timu kutoka kata ya Bukanda imeiadhibu timu ya kata ya Nakatunguru kwa magori 21 kwa 8 na timu kutoka kata ya Ngoma imetetea ushindi kwa kufunga magori 21 dhidi ya Kakerege aliyeambulia magori 19.
Michezo mingine itaendelea Aprili 25, 2024 ambapo itawakutanisha miamba kutoka kata ya Bukongo dhidi ya Watoto wa mjini Nansio
Nkilizya Vs Namagondo kwa mechi ya mpira wa Miguu na Pete.