Mazishi ya
aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ndala katika Jimbo Katoliki Shinyanga Hayati
Padre Emmanuel Makolo, yatafanyika wiki ijayo siku ya Jumanne tarehe
30.04.2024, katika makaburi ya Mapadre yaliyopo Kanisa kuu Ngokolo mjini
Shinyanga.
Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Paul
Mahona, mwili wa Marehemu utapokelewa mjini Shinyanga kutoka Bugando Jijini
Mwanza siku ya Jumatatu tarehe 29.04.2024, katika eneo la Ibadakuli na
utapelekwa moja kwa moja katika Parokia ya Ndala alipokuwa akifanya utume enzi
za uhai wake kwa ajili ya Misa ya kumwombea itakayoaanza saa 5:00 asubuhi.
Misa hiyo itafuatiwa na zoezi la kutoa heshima
za mwisho kwa waamini wa Parokia ya Ndala na watu wote wenye mapenzi mema na
baadaye usiku kutakuwa na jumla ya Misa nne za mkesha kwa ajili ya kumwombea
marehemu.
.
Mwili wa Marehemu utapelekwa katika katika
Kanisa kuu Ngokolo siku ya Jumanne saa 1:00 asubuhi, ambapo waamini na watu
wenye mapenzi mema watatoa heshima zao za mwisho kabla ya Misa ya mazishi
ambayo itaanza saa 4:00 asubuhi.
Padre Makolo amefariki dunia siku ya Alhamisi
tarehe 25.04.2024, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa
ya Kanda Bugando Jijini Mwanza.
Mungu ailaze mahali pema Mbinguni roho ya
Marehemu Padre Emmanuel Makolo...Amina.