Mtangazaji wa Clouds Gardner afariki Gardner maarufu kama Kapteni amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Dar es Salaam. Mtangazaji maarufu wa kituo cha redio cha Clouds FM, Gardner G Habash amefariki dunia. Msemaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Emilian Mallya amethibitisha kifo cha mtangazaji huyo.


Gardner, mtangazaji wa kipindi cha Jahazi amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo Aprili 20, 2024, saa 11 alfajiri.


“Ni kweli kwa taarifa za awali amefariki, lakini nitatoa taarifa zaidi baadaye,” amesema Mallya.

SOMA hapa zaidi Chanzo Mwananchi