Na Sebastina Mnakaya, KahamaZaidi ya nyumba 533 kata Igwamanoni Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga zimepata itilafu za maafa kwa kutengeneza nyufa na nyingine kuanguka baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku nne mfululizo na kusababisha wananchi kuondoka kwenye nyumba zao ili kuepuka maafa.Hayo yamesemwa na mratibu wa maafa Halmashauri ya Ushetu MINAELI NGOMOI wakati akikagua athari za mvua hizo katika makazi yalioathirika katika kijiji cha Luhaga, ambapo amesema kuwa kaya 141 zimeathirika zaidi ambazo zinahitaji maturubai na msaada pamoja na kuwataka watanchi wa meoneo hayo kuchukua tahadhari ya kuondoka ili wasipate madhara zaidi."Kuna maafa yametokea katika kata ya Igwamanoni ambapo Kuna kaya 533 ambazo hizo nyumba zimepata itilafu ya maafa lakini katika kata hiyo Kuna shule ya msingi Igwamanoni ambayo madarasa yake matano yamepata nyufa kutokana na mvua zinazonyesha, pia tumeshaanza kutoa tahadhari ya maafa hayo kwa kuwaelimisha wananchi kwa wale ambao nyumba zao haziko imara kutoendelea kukaa kwa kipindi hiki pamoja na kukimbilia kwenye maeneo ya mzuri ambayo hayajapata athari ikiwemo maeneo ya shule na ofisi za kijiji na kata" Minaeli NgomoiAkiwa katika eneo la tukio akikagua hali ilivyo kwa wananchi waliathirika, mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA amesema kuwa halmashauri iendelee kutoa elimu kwa wananchi namna bora za kujenga nyumba zao ambazo zitakuwa imara kutokana na ardhi ya maeneo hayo ili kupunguza athari za maafa yanapotokea."tunashukuru Mungu tumepata taarifa usiku lakini hapakuwa na majeruhi au vifo, lakini inaweza siku sasa ikatokea nyumba ikamwangukia mtu na hakuna namna ya kumsaidi na ndiyo maana pia tunazunguka na wataalu wa tarura kuangali miundombinu ya barabara, pia wananchi watakiwa kupewa elimu juu ya ujenzi bora wa nyumba zao kutokana na eneo husika kitaalam ili kupunguza majanga yatokanayo na maafa" amesema Mboni MhitaBaadhi ya wananchi wa kata hiyo walioathirika na mvua hizo wakizungumza kwa nyakati tofauti ANNA MAHANO amesema nyumba anayoishi imetengeza ufa na kusababisha kuhama kwa ajili ya usalama wake, huku BUNDALA JUMA ameiomba serikali kumsaida maturubai ili kuweza juu kusubiri kiangazi na aweze kujenga upya huku akiwa na familia ya zaidi ya watoto 10." Nimepata shinda ya kuangukiwa na nyumba yangu mpaka nikahama kwenda Iramba na mpaka sasa nahangaika sasa hivi sina mpa kulala " amesema Anna Mahano."Mvua ilinyesha zaidi ya masaa matano na baada ya kukatika ndani ya masaa mawili ilitengeneza nyufa na kuanguka, naomba serikali inisaidie maturubai ili niweze kuwezaka kwa muda ili familia yangu iwe salama" amesema Bundala Juma.Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Igwamanoni walioathirika na maafa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiendelea na ziara yake ya kutembelea na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Igwamanoni walioathirika na maafa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Igwamanoni walioathirika na maafa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Igwamanoni walioathirika na maafa.