MWILI WA MAREHEMU PADRE MAKOLO UMEPOKELEWA LEO JIMBONI SHINYANGA KWA AJILI YA MAZISHI HAPO KESHO

 

Mwili wa aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ndala katika jimbo Katoliki Shinyanga hayati Padre Emmanuel Makolo, umewasili jimboni Shinyanga kutoka Bugando Mwanza, kwa ajili ya taratibu za mazishi hapo kesho.

Mwili umepokelewa mchana wa leo na Mapadre, Watawa na waamini wakiongozwa na Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kwenye kanisa la kigango cha Ibadakuli Parokia ya Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga .

Baada ya  Ibada fupi iliyofanyika katika kigango cha Ibadakuli, mwili wa marehemu umepelekwa moja kwa moja katika Parokia ya Ndala alipokuwa akifanya utume enzi za uhai wake, ambapo pamoja na mambo mengine, Wakili Askofu Padre Kizito Nyanga ameongoza Misa takatifu ya kumwombea, ambayo pia imehudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya amani na Maridhiano ya Wilaya ya Shinyanga ambayo Hayati Padre Makolo alikuwa Mwenyekiti wake.

Baada ya Misa hiyo waamini wa Parokia ya Ndala pamoja na watu wengine wameendelea kutoa heshima zao za mwisho, ambapo kuanzia saa moja jioni zinafanyika Misa za mkesha takribani nne za kumwombea, kabla ya mwili huo kupelekwa Kanisa kuu la Ngokolo hapo kesho kwa ajili ya mazishi.

Padre Makolo alizaliwa mnamo Aprili 22 mwaka 1958 katika Kijiji cha Mwamagembe wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, ambapo baada ya masomo yake ya majiundo ya Kipadre, alipewa Daraja takatifu la Upadre mnamo Julai 2 mwaka 1987 katika Parokia ya Ndoleleji.

Padre Makolo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano wa Wilaya ya Shinyanga, alifariki dunia Alhamisi tarehe 25.04.2024, katika Hospitali ya rufaa ya kanda Bugando jijini Mwanza, alikopelekwa kwa matibabu.

Redio Faraja itarusha Mubashara (Live) kwenye Redio na kupitia ukrasa wa Face book (Radiofaraja tz) Misa ya Mazishi ambayo itaanza saa 4:00 asubuhi, itakayongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu

Mungu ailaze mahali pema Mbinguni roho ya Marehemu Padre Emmanuel Makolo…Amina

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo likishushwa kwenye gari mara baada ya kuwasili katika Kigango cha Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga na kupokelewa na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu

Wakili Askofu Padre Kizito Nyanga akiwa ameshika Msalaba

Maandamano kuingika kwenye Kanisa la Kigango cha Ibadakuli kwa Ibada fupi iliyoongozwa na Askofu Sangu

Padre Simon Maneno ambaye ni Mkurugenzi wa miito na Paroko wa Parokia ya Buhangija (Mwenye kanzu nyeupe) pamoja na Wakili Askofu Padre kizito Nyanga kwa kusaidiana na waamini wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu

Jeneza lenye mwili wa Marehemu linawekwa Kanisani katika Kigango cha Ibadakuli

Askofu Sangu akitoa Mahubiri mafupi na kuelezea kwa ufupi wasifu wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo kupitia Ibada fupi iliyofanyika kwenye Kigango cha Ibadakuli

Askofu Sangu akinyunyizia maji ya BarakaMwilli wa Marehemu

Askofu Sangu akifukiza ubani Mwili wa Marehemu

Msafara wenye Mwili wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo ukielekea kweye Kanisa la Mtakatifu Alberto mkuu Parokia ya Ndala

Mwili wa Marehemu ukipokelewa katika Parokia ya Mtakatifu Alberto Mkuu Ndala mjini Shinyanga

Mapadre wakiingiza Mwili wa Marehemu ndani ya Kanisa la Mt.Alberto mkuu Parokia ya Ndala, nyuma yao ni Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu

Paroko msaidizi wa Parokia ya Bukundi Padre Emmanuel Gembuya akisoma Historia fupi ya Marehemu Padre Emmanuel Makolo

Shemasi Philemon Nkuba wa Jimbo la Shinyanga akisoma Somo la Injili kwenye Misa ya kumwombea Marehemu iliyofanyika katika Kanisa la Mt.Alberto Mkuu Parokia ya Ndala

Mkurugenzi wa Kiroho kutoka Chuo kikuu cha SAUT Mwanza Padre Charles Bundu akitoa Mahubiri kwenye Misa, Padre Bundu ni Padre kutoka Jimbo la Shinyanga ambaye pia amefanya kazi kwa karibu na Marehemu Padre Emmanuel Makolo

Wajumbe wa Kamati ya Amani na Maridhiano Wilaya ya Shinyanga wakiwa Kanisani kwenye Misa ya Kumwombea Padre Emmanuel Makolo

Wanakwaya , waamini na watu mbalimbali wakiwa Kanisani

Katibu wa Kamati ya Amani na Maridhiano Wilaya ya Shinyanga Sheikh Shaban Katundu akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Kamati

Wakili Askofu wa Jimbo la Shinyanga Padre Kizito Nyanga akizungumza mara baada ya kuongoza Misa ya kumwombea Marehemu Padre Emmanuel Makolo

Wakili Askofu Padre Kizito Nyanga akitoa Baraka kwa waamini mara baada ya Misa

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo

Mama Suzana Mbuke Emmanuel ambaye ni Mama mzazi wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo (Mwenye kitambaa cheusi kushoto) pamoja na ndugu wengine wa Marehemu

Watu mbalimbali wakimfariji Mama Suzana Mbuke Emmanuel ambaye ni Mama mzazi wa Marehemu Padre Emmanuel Makolo

Previous Post Next Post