Aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Ndala katika Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Emmanuel Makolo, amefariki dunia.
Padre Makolo amefariki dunia Jana Alhamisi tarehe 25.04.2024 , majira ya saa tatu usiku, katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Jijini Mwanza alikopelekwa kwa matibabu.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika.
Mungu ailaze Mahali pema Mbinguni Roho ya Marehemu Padre Emmanuel Makolo….Amina