Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 29 Aprili, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau na Watekelezaji wa Mradi wa "CHAGUO LANGU HAKI YANGU" ambao ni WiLDAFtz, C-SEMA, HELP AGE TANZANIA, TGNP na TANZANIA INTERFAITH PARTNERSHIP wakiongozwa na Bi. Rashida Shariff ambaye ni Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu Duniani (UNFPA) pamoja na kuwakaribisha Mkaoni Shinyanga lakini pia amewaeleza kuwa Serikali itashirikiana nao katika kutekeleza mradi lengwa na akawaahidi ushiriiano wakati wote.
Haya yamesemwa leo walipofika Ofisini kwake kwa lengo la kujitambuli ambapo pamoja nalo lakini pia wapo katika ziara ya kutembelea maeneo ambayo mradi unatekelezwa ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Kahama na Kishapu.
"Nimefurahi sana kukutana nanyi hapa ofisini, nawapongeza sana kwa kazi zote mnazozifanya katika kuwahudumia na kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali wakiwemo na wananchi wa Mkoa huu wa Shinyanga, nami ninawaahidi ushirikiano wakati wote mtakapohitaji ili kufanikisha lengo la mradi katika Wilaya hizi mbili, karibuni sana wakati wowote," amesema RC Macha.
Kando na haya, pia wadau wameweza kumshirikisha kazi mbalimbali zinatekelezwa na mradi huu, mafanikio na mambo waliyojifunza katika maeneo ya utekelezaji wa mradi.