SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YATOA ELIMU YA UKATILI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HOPE

Na Mapuli Kitina Misalaba

Katibu wa kampeni ya kupinga ukatili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya amewataka wanafunzi kujiepusha na makundi mabaya huku akiwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuwa kielelezo bora katika jamii na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo wakati viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi katika shule ya msingi Hope iliyopo Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

Bwana Kapaya pamoja na mambo mengina amewahimiza wanafunzi hao kujiepusha na makundi mabaya ambayo yanaweza kusababisha ukatili katika maisha yao na kwamba amewataka kusoma kwa juhudi ili waweze kufikia malengo yao.

Mwenyekiti idara ya Itifaki, uanachama na uenezi Bwana Solomon Najulwa amewataka wanafunzi hao kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na uvutaji sigara.

Mwenyekiti wa idara ya Utamaduni, mila na destori Mwinjilisti Esther Emmanuel amewasisitiza kuepuka mila na desturi kandamizi huku akiwasisitiza kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao.

Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) ni kampeni ya kupinga ukatili ambapo katika Mkoa wa Shinyanga pamoja na mambo mengine imeendelea kuzishauri shule zote kuweka vibao vyenye maneno ya kukataa ukatili kwenye mazingira ya shuleni ili kuwaimarisha wanafunzi.Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Hope, Mashimba Lucas akizungumza.


Previous Post Next Post