Mkuu wa Takukuru Mwanza James Ruge amesema kupitia Takukuru Mkoa wa Mwanza kupitia kazi ya Uchambuzi wa Mfumo Wa Kodi ya Zuio imesaidia Sh 68,164,545 kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA ) kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela
Ruge amesema Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru)Mkoa wa Mwanza katika kipindi Cha Januari -March ,2024 imefuatilia utekelezaji wa Miradi 15 ya Maendeleo yenye Thamani ya 19,110,131,068.79/ Miradi hii imefuatiliwa fedha iliyotumika.Miradi lilihusishaSekta ya Afya,Maji, Elimu na Uchukuzi kati ya Miradi hiyo15 iliyofutiwa Miradi 7 imekutwa na Mapungufu Mbalimbali
Hata hivyo Takukuru Inaendelea kutekeleza Majukumu yake Kwa Mujibu wa Sheria.Hata hivyo mkakati uliopo katika kipindi Cha April - Juni 2024 kuzuia vitendo vya Rushwa kwenye utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Kwa kutoa Elimu Kwa Wananchi, kuisimamia Kwa karibu zaidi matumizi Sahihi ya Fedha zinazotolewa na Serikali Kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi pamoja na kuchunguza makosa ya Rushwa kuchukulia hatua wale wote watakaojihusisha na vitendo vya Rushwa Kwa Mujibu wa Sheria
Lakini pia Takukuru inatoa wito Kwa Wananchi kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Maeneo yetu .Kwa Pamoja tuzuie na kukemea vitendo vya rushwa katika Maeneo ya kupata huduma kwani ni jukumu letu sote wananchi