Na Mapuli Kitina Misalaba
Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa
kushirikiana na viongozi mbalimbali, wadau na wananchi leo asubuhi Aprili
25,2024 wamefanya usafi wa mazingira na kupanda miti 650 katika eneo la Hospitali
ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya muungano
wa Tanganyika na Zanziber.
Mgeni rasmi
katika shughuli ni katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akimwakilisha
mkuu wa Wilaya ya Shinyanga.
Pamoja na mambo mengina Bwana Kitinga ameikumbusha
jamii kuendelea kupanda miti katika maeneo yao kama sehemu ya kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi.
Pia ametoa wito kwa watanzania kuendelea kushikamana
na kushirikiana ili kuendeleza amani na usalama nchini.
Amesema ni vema watanzania kuendelea
kushikamana na kushirikiana katika
shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuendelea kuimarisha umoja na usalama wa
taifa.
Afisa maliasili na mazingira wa Manispaa ya
Shinyanga Ezra Manjerenga amesema miche ya miti 650 imependwa leo kama sehemu
ya maadhimisho ya miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber ambapo amesema
zoezi hilo ni endelevu.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga Dkt. Pierina Mwaluko ameahidi kuisimamia miti hiyo ili
iweze kuleta matokeo chanya.
Baadhi ya wananchi na viongozi mbalimbali ambao
wameshiriki shughuli ya upandaji miti wameeleza wataendelea kuunga mkono
kampeni ya upandaji miti katika jamii ambapo pia wameahidi kuendeleza amani na umoja wa taifa hili.
Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa
kushirikiana na viongozi mbalimbali, wadau na wananchi imefanya usafi wa
mazingira na kupanda miti katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber.
Kauli mbiu ya maadhimisho Miaka 60 ya muungano wa
Tanganyika na Zanziber Mwaka huu inasema “TUMESHIKAMANA, TUMEIMARIKA KWA
MAENDELEO YA TAIFA LETU”.
Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said
Kitinga akipanda mti kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga leo Aprili
25,2024 katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber.

Kitinga akizungumza baada ya kupanda mti kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Shinyanga leo Aprili
25,2024 katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber.
Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said
Kitinga akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya zoezi la upandaji miti leo asubuhi Aprili
25,2024 katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber.
Katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya zoezi la upandaji miti leo asubuhi Aprili 25,2024 katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanziber.