Asasi ya Vijana ya Youth - VDT yenye makazi yake katika Manispaa ya Shinyanga imeendelea kutoa msaada wa kofia kwa watanzania waishio na ulemavu wa ngozi katika Tarafa ya Mjini.Akiongea katika makabidhiano, Mratibu wa asasi hii Bwana Nicholaus Luhende ameeleza kuwa, wameona ni vema kuwafikia ndugu waishio katika jamii kwani mara nyingi husahaulika kwa kuwa hawako vituoni.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Masekelo, Ndugu Constantine Masalu ameshauri wadau wanaojihusisha na makundi maalum wajitahidi kuwaunganisha walemavu wa ngozi ili waweze kusaidika kujikwamua kiuchumi. Amependekeza ufugaji wa mifugo rafiki kwa mazingira yetu kama kuku wa kienyeji kwa walemavu walio wajasiliamali.Mratibu ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, Idara ya Ustawi wa Jamii kuweza kuwaunganisha na watendaji wa Kata za Lubaga, Masekelo, Mjini, Ndembezi na Ngokolo; pamoja na shule ya msingi Balina na Sekondari ya Wasichana ya Shinyanga ambako msaada huu ulifika. Na ametoa rai kwa Kata ambazo bado kuwasiliana pindi wanapopata wenzetu watakaohitaji kofia hizi maalum. Afisa Maendeleo ndugu Anna Magawa ameshukuru kwa msaada huo lakini pia amekumbusha ndugu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika jamii kujisajili kama vikundi katika Kata zao ili wakopesheke.Wanafunzi kutoka Shule ya Wasichana ya Shinyanga wameshukuru kupatiwa kofia hizi maalum na kwamba zitawasaidia wanapopambana na mionzi ya jua. Pia wamehimiza kupatiwa miwani za jua kwani zitasaidia kutunza macho yao.Unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mratibu wa Youth VDT kupitia namba +255783233333