MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA WAKILI
JULIUS MTATIRO ANAWAOMBA WANANCHI WOTE KUHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YATAKAYOFANYIKA KESHO TAREHE 25.04.2024.
MAADHIMISHO HAYO YATAKWENDA SANJARI
NA MATUKIO NA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII ZITAKAZOFANYIKA KUANZIA SAA 2.00
ASUBUHI.
1.SHUGHULI YA KWANZA ITAKUWA NI
KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA NA KUPANDA MITI KATIKA ENEO LA HOSPITALI YA MANISPAA
YA SHINYANGA.
2.TUKIO LITAKALOFUATA NI MDAHALO
UTAKAOFANYIKA KATIKA CHUO CHA UALIMU
SHINYANGA ( YAANI SHYCOM ).
3.ITAFUATIWA NA SHEREHE YA MAADHIMISHO YA MUUNGANO KATIKA UWANJA WA ZIMAMOTO
JIRANI NA SOKO LA NGUZONANE MJINI
SHINYANGA , AMBAPO WANANCHI WATAUNGANA
NA WATANZANIA WENGINE KUSIKILIZA HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, DKT. SAMIA SULUHU
HASSAN KUPITIA RUNINGA KUBWA
ZITAKAZOKUWA ZIMEFUNGWA KATIKA ENEO HILO
SANJARI NA BURUDANI MBALIMBALI.
MGENI RASMI ATAKUWA MKUU WA MKOA WA
SHINYANGA ANAMRINGI MACHA.
KWA TANGAZO
HILI WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO HAYO KESHO.