MWANAFUNZI anayehitimu kidato cha sita kwenye shule ya sekondari Loreto Jijini Mwanza ameapa kutimiza ndoto yake ili aweze kuwa mtatibu wa magonjwa ya akina mama na watoto kuondokana na magonjwa yanawasibu.
Pendo Paul (19) anayesoma Mtaala wa masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia (PCB) ambaye aliibuka mwanafunzi bora kwa kidato cha sita ambawo karibia waanze mitihani ya kumaliza elimu hiyo alisema anatamani aweze kutimiza ndoto yake hiyo.
Alisema makundi hayo yanakabiliana na maradhi yanayojitokeza mara kwa mara hivyo anatamani awe kuwa mbobevu kwenye tiba ya maradhi hayo ili aweze kuwasaidia kwa ushauri wa kitaalamu na kuwatibu kwa umakini ili atimize adhima yake ya kuhakikisha kuwa wanaishi kwa usalama zaidi.
"Kufanya vizuri kwangu kumetokana na kumpenda Mungu vilevile kuwa na nidhamu kwa watu wote"alisema Paul.
Mshauri wa Masuala ya Elimu wa Shirika la Universities Abroad Representative (UAR) Tony Kabetha alisema kunahitajika ushauri kupewa wanafunzi ili waweze kuendelea kusomea masomo yenye fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.
Alisema wanajitahidi kuwatafutia wanafunzi wa kitanzania vyuo mbalimbali nje ya nchi ili taifa liweze kupata kada ya watumishi watakaoweza kuletea nchi mapinduzi ya kijamii na kisayansi ili tufikie maendeleo endelevu.