Timu ya Bugweto FC
kutoka kata ya Ibadakuli imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi
walioupata kupitia mikwaju ya penati katika michuano ya Salome Makamba Cup
inayoendelea kutimua vumbi hatua ya robo
fainali .
Bugweto FC
waliwakaribisha jirani zao timu ya Mwagala FC kutoka kata ya Kolandoto katika
mchezo wa hatua ya pili (robo fainali) na kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya
Penati 6 – 5 baada ya kufungana goli 2-
2 ndani ya dakika 90.
Mwagala FC walitangulia
kupata goli kipindi cha kwanza kupitia kwa Zabrone Ngassa baadae Nkwano Deusi wa Bugweto FC
alisawazisha goli hilo dakika za mapema kipindi cha pili kisha Renald wa timu
ya Mwagala FC alipachika goli la pili ambapo baadae Frank Samweli
aliisawazishia Bugweto FC na kumalizika kwa dakika 90 kwa sare ya goli 2 – 2.