CDF MKUNDA AELEZA UMUHIMU WA JKT KATIKA ULINZI WA TAIFA

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akikagua gwaride kabla ya kufunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba

MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati alipofunga mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi la Ulinzi Tanzania Brigedia Jenerali Abubakari Charo akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba

Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba.

MKUU wa Kikosi cha Jeshi 838 JKT Maramba Kanali Ashraf Hassan akizungumza wakati wa mafunzo hayo



Na Oscar Assenga,MKINGA.


MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob Mkunda amesema mafunzo ya awali ya ya Kijeshi kwa vijana wa kujitolea Operesheni miaka 60 ya JKT kikosi cha Jeshi 838 Maramba huku akieleza umuhimu wa vijana hao ni mkubwa kutokana na kwamba wanaingia kwenye Jeshi la akiba ambalo inapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa wanaitwa kwa mujibu wa sheria.

Jenerali Mkunda aliyasema hayo Jumanne Aprili 30 mwaka huu wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ambapo aliwakilishwa na Brigedia Jenerali Abubakari Charo ambapo alisema kutokana na miongozo mbalimbali iliyopo kwa mafunzo hayo ya vijana hasa kwa kuzingatia kwamba vijana hao wanapohitimu mafunzo yao wanaingia kwenye jeshi la akiba.

Alisema kwamba linapotokea hitajiko la ulinzi wa Taifa na Rais na Amri Jeshi Mkuu akatangaza hali ya hatari vijana hao wanaitwa kwa mujibu wa sheria kwenda kuungana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kulinda ulinzi wa Taifa.

Aidha alisema kutokana na umuhimu wa vijana kwenye Jeshi hilo wanapenda kuona wanafikia viwango na malengo ya mafunzo hayo na amewaona wamefikia viwango vinavyotakiwa huku akieleza yanawajenga kwenye nidhamu, ukakamavu, uzalengo, uhodari wa kujiamini na kulipenda taifa lao.

“Nichukue fursa hii kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kutoa shukrani kwa dhati kwa Serikali kwa juhudi zinazofanyika kuhakikisha mazingira ya mafunzo kwa vijana ndani ya JKT yanaboreshwa”Alisema

“Kwani katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imetoa kiasi cha sh Milioni 950 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwa vijana wanaojiunga na JKT fedha hizo zimeweza kujenga mabweni 12 kila moja lenye uwezo wa kuchukua vijana 120 hivyo kusaidia kikosi kuongeza uwezo kuchukua vijana 1440 na hii ni ishara za wazi kwamba serikali inatambua na kuthamini mafunzo ya vijana wa JKT”Alisema

“Lakini pia ujenzi wa vyoo vitano ambapo kila choo kina matundu 22 vitatumika kwa vijana hilo sio suala dogo ni jambo kubwa ambalo serikali imefanya kwa mazingira hayo wanawaomba vijana ambao hawapati fursa kujiunga na JKT wasije kufikiria wametengwa na kunyimwa fursa bali lengo vijana wote wapite Jkt na wale vijana wanaomaliza kidato cha sita”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Jeshi la Kujenga Taifa litakuwa likiendelea kuongozewa uwezo huku akieleza wanathamini juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya jeshi hilo ambapo mafunzo ambayo wameyapata yatawawezesha kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama,sekta mbalimbali za serikali au makampuni mbalimbali .

Awali akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema mafunzo hayo kwa vijana wa JKT ni muhimu sana kwa vijana kwa maana wao ndio tegemeo la Taifa.

Balozi Batilda alisema Rais Dkt Samia Suluhu kupitia falsafa yake ya 4R ameendelea kusimamia na ndio maana juzi chadema walikuwa na maandamano yao wakasimamiwa vizuri na jeshi la Polisi wakafanya mkutano wao wakatembea.

Alisema kwa hakika wakawa na matumaini watapata mambo ya msingi yatakayowasaidia kujenga nchi lakini wakasikia mambo tofauti kwanini wakuu wa mikoa hawapigiri kura, kama madiwani sasa akasema hata RC akipigiwa kura atachaguliwa Tanga na RC ni msaidizi wa Rais anaweza kuhamishwa kila eneo .

“Tulitegemea kwamba hivi sasa nchi ipo kwenye kipindi kigumu na mvua zinanyesha madhara maeneo mengi barabara nyingi zimepata changamoto na maeneo mengi lami zimepasuka changamoto ni nyingi vita vya israel vinaendelea duniani gharama zinapanda bei ya dola ipo kubwa kulingana na bei yetu sisi tukaona haja hoja zao za za kwamba hazikuwasaidia wakapata mawazo mbadala hazipo"Alisema

Hata hivyo Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Elias Sikaponda alisema kwamba alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa sababu yanaleta tija kwa vijana katika shughuli za kujitegemea huku akiwataka kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya

Aliwataka pia vijana hao kutumia elimu waliyoipata wakaweze kutatua changamoto mbalimbali pasipo kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa hapa nchini huku akisiistiza watumie nidhamu pekee kama silaha kwenye jambo lolote mbeleni.
Previous Post Next Post