TAARIFA
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) anawataarifu wateja na Wadau wote kuwa mawasiliano na wenzetu wa KASHWASA yamefanyika na tayari matengenezo yamekamilika na hatua ya kwanza ni kujaza tanki kuu la Maji lililopo Mabale katika wilaya ya Misungwi,
hivyo kwa Manispaa yetu tutarajie huduma ya maji kuanza kuingia kwenye Tanki letu kuu la Old Shinyanga kesho asubuhi.
Mamlaka inaendelea kuzalisha huduma ya majisafi kupitia chanzo cha Maji toka bwawa la Ninghwa.
Maeneo yanayopata huduma kwa sasa ni Mwalugoye, Bushushu, kambarage,Mwasele ,
Lubaga pamoja na maeneo ya Butengwa.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
Taarifa imetolewa na kitengocha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma - SHUWASA