DC KATWALE AWATAKA WATOA HUDUMA KWENYE MABASI KUZINGATIA UBORA NA USALAMA KWENYE KAZI YAO

 Na  Lucas Raphael,Tabora

 

Mkuu wa wilaya ya Tabora  Deusdedith Katwale amewataka watoa huduma kwenye Mabasi kuzingitia Sheria kanuni na  taratibu za usafirishaji wa Abiria Ili kutoa huduma Bora Kwa wasafiri.

 

Kauli hiyo ilitolewa wakati akifungua  mafunzo kwa wahudumu wa mabasi ya masafa marefu  na mjijni katika kanda ya magharibi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mtemi Isike Mwanakiyungi  mkoani Tabora.

 

Mafunzo hayokwa wahudumu hao wa Mabasi yatatolewa Kwa siku Tano  mkoani hapa chini ya wataalum wa  chuo Cha Taifa Cha usafirishaji wakishirikiana na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA

 

Katwale alisema kwamba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga Zaidi ya Shilingi Bilion 49 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya usafiri Kwa watanzania Ili waweza kusafiri salama bila changamoto yoyote .

 

Aidha alitaka mafunzo hayo yakawe chachu ya mabadiliko kwenye sekta ya usafirishaji wa Abiria na kuifanya huduma hiyo Kuwa Bora kama  huduma za usafiri wa Anga.

 

Katwale aliwaasa wamiliki wa vyombo vya usafiri kushirikiana na watoa huduma Ili Kuifanya huduma Hiyo Kuwa Bora Ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Mabasi yanakuwa na ubora wa Hali ya juu  na sio Kuwa  Mabasi mabovu ambayo yatakuwa kero Kwa wasafiri 

 

Kwa Upande wake mkuu wa kituo cha Umahiri katika usafiri wa Anga na Oparesheni za usafirishaji kutoka chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji Dkt Chacha Ryib   alisema Lengo la mafunzo hayo ni kuboresha huduma zinazotolewa kwenye Mabasi zifanane na huduma zinazotolewa kwenye vyombo vingine vya usafiri kama Ndege na Meli.

 

Alisema kwamba mafunzi hayo tayarai yamewanufaisha zaidi wa wahudumu wa mabasi wapatao 423 nchini nzima toka walipoanza kutoa mafaunzo hayo katika kanda sita .

 

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa LATRA Nchini Nelson Mmari ambaye ni Afisa mfawidhi wa LATRA mkoani Tabora amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri wa mabasi kuhakisha watoa huduma wa ndani ya Mabasi wawe wamepata mafunzo yanayotolewa na mamlaka husika na adhabu itatolewa Kwa chombo husika endapo ikagundulika mhudumu Hana mafunzo ya usafirishaji.

 

Alifafanua kwamba mamlaka inajukumu la kusajili wahudumu na kuwathibiti madereva wa vyombo vya maoto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara .

 

Hivyo ni muhimu wa miliki wa mabasi nchini kuhakikisha inawahudumu waliopata elimu ya kuhudumia kwenye mabasi hayo na kama basi litakutwa halina hudumu aliyesajili faini itahudusu”alisema Mmari

Previous Post Next Post