Wakili Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Padre Kizito Nyanga, leo Ijumaa tarehe 03.05.2024, ataongoza Misa ya kumwombea aliyekuwa Paroko wa parokia ya Ndala Marehemu Padre Emmanuel Makolo, ambayo itafanyika katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianey Mhunze Wilayani Kishapu.
Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianey Mhunze ndiko nyumbani alikozaliwa Hayati Padre Makolo.
Kwa Mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, Misa hiyo ambayo pia itahudhuriwa na Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, itaanza saa 4:00 asubuhi na itahudhiriwa Mapadre, watawa na waamini kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Jimbo.
Padre Makolo amefariki dunia mnamo Aprili 25 mwaka 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Jijini Mwanza na amezikwa Jumanne Aprili 30 katika makaburi ya Mapadre yaliyopo Kanisa kuu Ngokolo mjini Shinyanga.
Mungu ailaze mahali pema Mbinguni roho ya Marehemu Padre Makolo..Amina