Kampuni Ya Lacuna Inayofanya Kazi zake ndani ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kama watoa huduma ya Shughuli Mbalimbali kama Ufundi Mitambo na Usambazaji wa Vipuli vya Magari.
Imetoa Msaada wa Magodoro 20 kwaajili ya wagonjwa wanaopatiwa Matibabu katika kituo cha afya Bugarama kinachopatikana Halamshauri ya Msalala, wilaya ya kahama Mkoani Shinyanga.
Akizungumza baada ya kukabidhi Masaada huo Mkurugenzi wa LACUNA COMPANY Amesema Wameamua kuunga juhudi za serikali kwa Kutoka Magodoro hayo kwani serukali tayari Imefanya mambo makubwa kama kuongeza wodi mbalimbali katika kituo hicho.
Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bugarama Dkt. Beatha Kahikye Ameishukuru sana Kampuni ya Lacuna kwa kutoa Msaada huo huku akiupongeza pia Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwahimiza watoa Huduma wao wanarudisha kile wanachopata kwenye Jamii.