MAMBO MANNE (4) YA KUYATAZAMA ILI KUPATA NA KUKUZA

 

Kuna wakati mwingine watu wengi huwa tunakosea sana kwa kutazama na kufikiri ya kuwa mtaji ni pesa peke yake  kwa ajili ya kufanzisha biashara. Kumbe kuna vitu vingine  ambavyo ni vya kuvitazama ili huo mtaji uweze kukua na kufanya kile ambacho unakihitaji ili kutimiza malengo yako.

Leo katika makala hii nitakwenda kukueleza kinaga ubaga ili uweze kufahamu ya kwamba kabla ya kuwa na mtaji ni lazima ujue misingi hiyo itakayokusaidia kutimiza ndoto zako. Kwani endapo utakosa misingi hiyo hata ukiwa na mtaji kiasi gani biashara utayoishazisha haitaishi miaka mingi.
Yafuatayo ndiyo mambo ambayo mtu anayahitaji ili kupata  na kukuza mtaji;

Akili
Kisaikolojia binadamu wote wana akili ila tatizo linakuja katika  uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Kimsingi ni kwamba watu wengi wanashindwa kutimiza malengo yao kwa sababu ni watu wavivu wa kufikiri. Watu wengi wanashindwa kugeuza maarifa waliyo nayo yawe bidhaa au huduma.

 Kwa mfano mtu anayefanya  biahara ya kupika chakula  na kupata kipato, mtu huyu hawezi kufikiri kufungua darasa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi waweze kupika  nay eye aweze kupata kipato zaidi. Tatizo linakuja ulichonacho hutaki kukifanya kikuongezee kipato zaidi. Ukitaka kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo jambo la msingi ni fikiri chanya kwa kubadili mtazomo ulionao.

Nguvu.
Hapa sizungumizii nguvu ya kuwa na misuli ya kupigana bali nazungumzia Ili uweze kuwa kile unachokitaka lazima utumie nguvu ulizonazo katika kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuzalisha huduma na bidhaa bora.  Watu wengi tuna hulka ya kuwa wavivu katika kufanya kazi na hii inatupelekea tunazidi kuwa ni watu wakutumia kuliko kuzalisha.  Wakati mwingine tunalalamika ya kuwa maisha ni magumu huku tukisahau kuwa sisi ndio wagumu katika katika kufanya kazi. Jambo la msingi ni kwamba badili mtazamo kwa kutumia nguvu ulizonazo katika kuzalisha kuliko kutumia tu.

Kipaji
Katika maisha ya mafanikio kuna vitu viwili. Kitu cha ambacho unatakiwa kufahamu ya kwamba ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na machaguo mawili yaani plan A na plan B ili uweze kufanikiwa. Mpango wa kwanza ni jinsi gani unaweza kutumia ujuzi ulionao ili kufanikiwa na mpango wa pili ni jinsi gani ya kutumia kipaji ulichonacho ili uweze kutimiza ndoto zako. Watu wengi hawaviishi vipaji vyao kwa sababu ya sababu mbalimbali.

Kwa mfano jiulize wakati ukiwa mdogo ulikuwa unapendelea kufanya nini zaidi?  kama umefikiliria kwa umakini  utakuwa umepata jibu  na je kitu hicho bado unacho au unafanyia kazi katika kukufanya ndoto ziwe kweli?  Ukifikiria kwa umakini utagundua ni kwamba watu wengi hatuna vipaji hivyo tena . Lakini tafiti nyingi zinaonesha ya kwamba watu ambao wanatuzunguka ndio ambao wanasabibisha kufa kwa vipaji hivyo.

 Nasema hivo nikiwa na maana ya kwamba watu wanaotuzunguka wakituona tunafanya jambo Fulani , watakukemea na kukuambia achaa! hicho kitu unachokifanya kitakufanya ushindwe kusoma na sababu nyingine nyingi ambazo hazina ukweli ndani yake.

Ila laiti kila mmoja angetumia vizuri kipaji chake alichopewa na mwenyezi Mungu  katika maisha yake walalamikaji tungepungua ambao huwa tunasema maisha ni magumu na tungepata mafanikio zaidi. Kumbuka kutumia kipaji ulichonacho ili kuongeza wigo mpana wa kupata kiapto ili kutimiza ndoto zako.

Ubunifu.
Kila kitu kinahitaji ubunifu ili kuona kina tija katika maisha yetu. Kwa kila jambo ambalo ulifanya linahitaji ubunifu. Ubunifu amabao nina uzungumzingia siku ya leo ni ule wa kutengeneza kitu kipya au huduma au kuongezea thamani katika kitu ambacho tayari unakifanya.

Ili kuongeza thamani  na kuapata kile unachokihitaji jaribu kuwa ndio mtu wa kwanza muundaji wa kitu hicho. Katika jambo hili unaweza kutumia kipaji ulichonacho kuwa mbunifu. Ubunifu ni lazima uwe wa peke yako. Ili kuweza kutimiza ndoto zako za kimafanikio jaribu kuyatazama mambo kwa jicho la tatu.

Wewe ambaye umesomea kuwa  mhasibu  ili kuweza kufanikiwa zaidi ni lazima ufikiri zaidi ya kuwa mhasibu kwa kuwa mbunifu ili uweze kutimiza malengo yako ambayo umejiwekea. Kuishi kwa kutengemea mshahara au hicho unachokifanya kukuingizia pesa hakikotoshi fikiri nje ya box kwa kuwa mbunifu zaidi ama hakika utafanikiwa.

Asante sana kwa kusoma makala hii mpaka kufikia hapo sina la zida tukutane tena katika makala ijayo ili kuweza kujifunza zaidi.

Na. Benson chonya
Previous Post Next Post