Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Paschal Patrobas Katambi, amekabidhi Magari matatu kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga- Mwawaza.
Magari hayo ni Gari la kubebea Wagonjwa (Ambulace) Gari la usimamizi shirikishi (Utawala) na Basi kwa ajili ya kuwachukua na kuwarudisha nyumbani watumishi.
Akikabidhi Magari hayo, Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, ameahidi kushirikiana na Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya Afya katika mkoa wa Shinyanga, ikiwemo kuongeza gari la wagonjwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga pamoja na kukijenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye kilomita 7, kinachoanzia eneo la Ndala kuelekea katika Hospitali hiyo, ili kuondoa adha kwa wananchi.
Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa kuwezesha miradi mingi katika mkoa wa Shinyanga, na hasa inayogusa maisha ya watu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha unatunza vifaa tiba na magari yanayotolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau, huku Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akisisitiza Magari yaliyokabidhiwa yatumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt.Luzila John, aliishukuru Serikali na wadau kwa kuendelea kuiwezesha hospitali hiyo kupata vitendea kazi na amemuomba Mheshimiwa Katambi kuendelea kusaidia upatikanaji wa mahitaji mengine ikiwemo kuboresha miumbombinu ya barabara inayotokea Ndala kuelekea Hospitalini hapo.
Muonekano wa Magari ambayo yamekabidhiwa na Mheshimiwa Katambi
Mheshimiwa Katambi akiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mheshimiwa Katambi baada ya kupokelewa na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John (mwenye suti ya kijivu kushoto)
Mheshimiwa Katambi akisalimiana na wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi Magari, mbele yake mwenye kofia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko
Baadhi ya Madiwani kutoka Kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga waliohudhuria Hafla hiyo wakimpokea Mheshimiwa Katambi
Madiwani wakiwa wamekaa
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akitambulisha wageni
Utambulisho ukiendelea
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Anold Makombe akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Luzila John akisoma Risala kwa Mgeni rasmi
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwa niaba ya Manispaa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwa niaba ya Serikali
Hafla inaendelea
Mheshimiwa Katambi akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi Magari
Mheshimiwa Katambi akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwa kazi nzuri anazozifanya katika Wilaya ya Shinyanga
Katambi akiendelea kuzungumza
Mheshimiwa Katambi na msafara wake wakielekea kwenye eneo yalipo Magari kwa ajili ya zoezi la kukabidhi
Mheshimiwa Katambi akikata utepe ishara ya kukabidhi rasmi Magari hayo kwa uongozi wa Hospitali rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Shangwe zikiendelea baada ya Mheshimiwa Katambi kukata utepe
Mheshimiwa Katambi akiteta jambo na baadhi ya viongozi
Mheshimiwa Katambi akiwasha Gari ishara ya kulizindua rasmi tayari kwa shughuli za Hospitali
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Matatiro kwa kushirikiana na Mheshimiwa Katambi wakikata utepe kuzindua Gari la Wagonjwa
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko kwa kushirikiana na Mheshimiwa Katambi wakikata utepe kuzindua Gari la Utawala
Picha ya pamoja na uongozi wa Hospitali