Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Paschal Patrobas Katambi, kesho atakabidhi Magari matatu kwa ajili ya Shughuli mbalimbali katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga- Mwawaza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Hospitali hiyo Bw. George Mganga, hafla ya kukabidhi Magari hayo itaanza saa 9:00 Alasiri, katika uwanja wa Hospitali.
Magari yatakayokabidhiwa ni pamoja na Gari la kubebea Wagonjwa (Ambulace) Gari kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Utawala na Gari kwa ajili ya kuwachukua na kuwarudisha nyumbani watumishi.
Baada ya kukabidhi Magari hayo, Mheshimiwa Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, atazungumza na watumishi kutoka Idara mbalimbali za Hospitali hiyo.