MICHUANO YA SALOME MAKAMBA CUP INAENDELEA KUTIMUA VUMBI TIMU TATU ZATANGULIA ROB0 FAINALI



Michuano ya Salome Makamba Cup inaendelea kutimua vumbi hatua ya pili ambapo timu za Bugweto FC, Mwagala FC pamoja na Chipukizi FC zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi katika michezo yao ya hatua ya pili.

Bugweto FC wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya Penati 3 – 2 dhidi ya Mwadui United FC baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya kufungana goli 4 – 4 ambapo Mwadui United FC walikuwa wa kwanza kupata goli dakika za mapema kipindi cha kwanza lakini safari yao haikufika kilele cha furaha kwa kuondolewa katika michuano hiyo kwa mikwaju ya Penati.

Timu nyinginge zilizofuzu ni Chipukizi FC waliopata ushindi wa goli 1 – 0 dhidi ya Home boys FC na kupata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali katika michuano ya Salome Makamba Cup pamoja na Mwagala FC waliofuzu kwa mikwaju ya Panati 3 – 2 kufuatia sare ya goli 1 – 1 ndani ya dakika 90 dhidi ya timu ya Mchicha FC.

Leo Jumamosi ya tarehe 25.05.2024 michezo miwili itachezwa katika viwanja tofauti tofauti ambapo majira ya saa 9:30 mchana Ngokolo Stars watawakaribisha Town Stars katika uwanja wa Boko uliopo kata ya Ndembezi na mchezo wa pili utachezwa katika uwanja wa Veta Shinyanga kwa kuwakutanisha Katunda FC dhidi ya Boko FC majira ya saa 9:30 mchana.

Michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Mh. Salome Makamba ambapo zawadi za washindi zitakabidhiwa Jumamosi ya tarehe 01.06.2024 katika uwanja wa Sabasaba uliopo Kambarage mjini Shinyanga, baada ya mchezo wa fainali kumalizika.

Wachezaji wa timu ya Mwagala FC na Mchicha FC wakisikiliza maelekezo kabla ya mchezo kuanza

Katibu wa Mbunge ambaye pia ni mratibu wa mashindano hayo Bw. Justine Mboya (mwenye suruali) akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo na wawakilishi wa wachezaji

Wachezaji wa timu ya Mchicha FC kutoka Kata ya Kolandoto katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza

Wachezaji wa kikosi cha Mwagala FC kutoka Kata ya Kolandoto katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza

Winga wa timu ya Mchicha FC akiwania mpira katikati ya mabeki wawili wa timu ya Mwagala FC katika dimba la Bugweto

Mashabiki wa timu ya Mchicha FC wakishuhudia burudani wakati mechi ikiendelea

Mshambuliaji wa timu ya Mwagala FC jezi namba kumi (10) mgongoni akijaribu kuwatoka walinzi wa timu ya Mchicha FC katika dimba la Bugweto

Mashabiki wa timu ya Mwagala FC wakishuhudia burudani wakati mechi ikiendelea Uwanja wa Bugweto

Kikosi cha timu ya Chipukizi FC kutoka Kata ya Ngokolo katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza katika uwanja wa Boko

Kikosi cha timu ya Home boys FC kutoka Kata ya Chamuguha (kwa Meya) katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza katika uwanja wa Boko

Wachezaji wa timu ya Chipukizi FC, Home boys FC wakipeana mikono na Waamuzi kabla ya mchezo kuanza

Mchezaji wa Chipukizi FC akiwa katika umiliki wa mpira wakati mchezo ukiendelea

Mshabiki wakiendelea kupata burudani ya mchezo ndani ya uwanja wa Boko

Picha ya wachezaji wa Chipukizi FC baada ya kufuzu robo fainali kufuatia ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Home boys FC mchezo uliochezwa katika uwanja wa Boko

Previous Post Next Post