Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwanaume mmoja aliyetambuliwa kwa jina la MANOTA JIDAIRIFA mwenye umri wa Miaka 45 mkazi wa mtaa wa Mazinge katika Manispaa ya Shinyanga, amekutwa akiwa amefariki Dunia kando kando ya reli ya kati eneo la Mazinge.
Tukio hilo limetolea leo mchana Mei 27,2024 baada ya mwanaume huyo kukutwa amefariki katika eneo
la relini mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi Mkoani Shinyanga.
Agnes Jidairifa ambaye ni dada yake na marehemu ameeleza kuwa
Manota amefililiza wiki moja akinywa pombe ya kienyeji aina ya Gongo na kwamba
alikuwa anakataa kula chakula nyumbani hali ambayo inatajwa kusababisha kifo
chake.
“Yaani kaka
yangu amekunywa Pombe kwa mfululizo wiki nzima kabisa nilijitahidi kumwambia
kwanini unayanywa kwa fujo hivi na ukiyanywa mpaka unakuja nayo nyumbani ya
nini, tukiivisha ukimtengea chakula anafinya kidogo tu anaacha ile juzi alikuja
muda wa saa tisa nikamuuliza umekula akasema hajala nikasonga ugali nikampa na
penyewe akajaribu kidogo tu akauacha akaenda kuyafuata tena mapombe akarudi
amelewa nikamwambia kula sasa akasema nitakula tu”.
“Jana pia
aliamka asubuhi akaenda vizuri muda wa saa tisa akarudi tena yaani alirudi hata
sauti yake iko mbali ugali kwa kweli hakuuweza ndo tukakoroga uji, leo tena asubuhi
tumekoroga uje umeshaiva sasa amenawa tu
akatoka akaenda tena nikamwambia kaa unywe uje kwanza ndo uende unakoenda akasema
mnanichelewesha sasa tumekaa muda ndiyo tumekuja kuitwa na watu kwamba twende
huku kumbe ameyanywa mapombe wakati anarudi alipofika relini kabla hajavuka
akawa amekaa hapo kwenye jua nafikiria namapombe ndo yakazidi kumaliza ngumu
mwili, mimi nilipoijiwa nikakuta hali kama hiyo sasa”.amesema Agnes
Baadhi ya majirani katika familia hiyo ya marehemu wameiomba
serikali kuchukua hatua kali kwa watu wanaouza pombe haramu huku wakiwasisitiza
hasa vijana kuacha kutumia pombe hiyo.
Wananchi hao wamesema matukio ya namna hiyo yamekuwa yakijitokeza
mara kwa mara ambapo wamesisitiza serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu
wanaofanya biashara ya pombe bila kibali.
Misalaba Media imezungumza na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga
kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi amekili kupokea
taarifa za tukio hilo ambapo amesema jeshi la Polisi linaendelea kufanya misako ili kuwakamata na
kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaouza pombe haramu.
“Jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga majira ya saa saba mchana leo
Mei 27,2024 tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi kwamba maeneo ya mtaa wa
Tambukareli kata ya Ndembezi tarafa ya mjini ndani ya Wilaya na Mkoa wa
Shinyanga alikutwa mtu mwenye jinsia ya kiume akiwa amefariki ambaye
amejulikana kwa jina Manota Jidailifa kwamba alikutwa akiwa amefariki na
inasadikika ni baada ya kunywa pombe kali kupita kiasi jeshi la Polisi baada ya
kupata taarifa tumefika kwenye eneo la tukio na tayari mwili umechukuliwa na
kupelewa Hospitali baada ya hapo mwili utakabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi”.
“Sisi bado tunaendelea na suala
la uelimishaji na ndiyo maana hawa polisi kata walioko kwenye kata wanafanya mikutano
na wananchi pamoja na mimi mwenyewe kamanda wa Mkoa tunawapa elimu wananchi
suala la pombe kali pombe aina ya gongo ni pombe ambayo ni haribifu lakini pia
inazoofisha afya na sisi tunaendelea
kufanya misako na doria kuhakikisha kwanza hili suala linakaa sawa”
“Lakini suala linguine sasa
tunakuja kwa hao vijana ni malezi kwahiyo wazazi, sisi jeshi la polisi, ustawi
wa jamii na taasisi mbalimbali sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba suala la
malezi tunalisimamia kuanzia ngazi ya familia kwahiyo viongozi wa dini na wananchi
tutoke kwa pamoja tukiwa kama wazazi au walezi kuhakikisha kwamba kizazi hiki
cha hawa vijana ambao wameibukia kwenye matendo ya hovyo hovyo tunakemea sote
kwa nguvu moja”.amesema SACP Magomi
Agnes Jidailifa ambaye ni dada yake na marehemu akizungumza na Misalaba Media
Baadhi ya majirani wakiwa katika familia ya marehemu.
Eneo ambalo marehemu amekutwa akiwa amefariki.
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi.