Timu za Ngokolo Stars na Magereza FC zimefanikiwa kutinga hatua ya pili katika michuano ya kuwania kombe la Salome Makamba, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 2 – 2 na kulazimika kwenda mikwaju ya Penati iliyomalizika kwa Ngokolo Stars kuibuka na ushindi wa 3 – 2.
Licha ya kichapo cha mikwaju ya Penati Magereza FC wametinga hatua ya pili ya michuano hiyo kikanuni (Best loser)
Timu hizo zinaungana na timu nyingine 10 zilizotangulia katika hatua ya pili ambazo ni Mwagala FC, Mchicha FC,Bugweto FC, Mwadui United FC, Chipukizi FC.
Timu nyingine ni Home boys, Katunda FC,Boko FC, Town Stars pamoja na Shinyanga Veteran FC.
Hatua ya pili itaanza kutimua vumbi siku ya kesho kwa michezo miwili itakayochezwa katika uwanja wa Bugweto ambapo mchezo wa kwanza utawakutanisha Mwagala FC dhidi ya Mchicha FC majira ya 8:00 mchana na mchezo wa pili utawakutanisha wenyeji Bugweto FC watakaoshuka dimbani dhidi ya Mwadui United FC majira ya saa 10:30 jioni.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Mh. Salome Makamba ambapo zawadi za washindi zitakabidhiwa Jumamosi ya 01.06.2024 katika uwanja wa Sabasaba uliopo Kambarage mjini Shinyanga, baada ya mchezo wa fainali kumalizika.
Wachezaji wa timu ya Magereza wakiwa katika picha ya pamoja
Wachezaji wa timu ya Magereza FC (kushoto),Waamuzi (katikati) pamoja na wachezaji wa timu ya Ngokolo Stars (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja
Wachezaji wa timu ya Ngokolo Stars wakiwa katika picha ya pamoja
Wachezaji wa timu ya Magereza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo
Waamuzi pamoja na viongozi wa timu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa Mbunge Bw. Justine Mboya (mwenye suruali)
Waamuzi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu (Captain)