Ticker

6/recent/ticker-posts

PACESH NA WADAU WA HAKI JINAI WAJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO KATIKA UPATIKANAJI WA HAKI JINAI


Shirika la msaada wa kisheria la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH) lenye makao yake makuu Mkoani Shinyanga, leo Alhamisi tarehe 30.05.2024,  limewakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya  haki jinai katika wilaya ya Shinyanga, ili kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto zilizopo  katika upatikanaji wa haki Jinai.

Wadau hao ambao ni pamoja na Maafisa wa Mahakama, Jeshi la Polisi, Ofisi ya taifa ya Mashtaka, Jeshi la Magereza, Wasaidizi wa kisheria, Maafisa maendeleo ya jamii, maafisa ustawi wa jamii, wataalam wa afya, wanaharakati wa kupinga ukatili na wawakilishi wa Asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya kutetea haki za wanawake na watoto,  wamekutana katika ukumbi wa Mahakama kuu kanda ya Shinyanga kupitia kikao maalum cha uzinduzi wa mradi uliopewa jina la Mwanamke salama , ambao utatekelezwa na PACESH katika Kata za Ndembezi na Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Kata ya Didia katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza katika Kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa PACESH Bw. John Shija, amesema mradi wa Mwanamke salama ambao umefadhiliwa na Shirika la kuwezesha huduma za kisheria la Legal Service Facility (LSF) ambao utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mzima, unalenga kuboresha huduma za kisheria hasa kuwezesha mashauri yanayohusu masuala ya ukatili kwa wanawake na wasichana, ambayo yamekuwa yakisuasua kutokana na changamoto zilizopo katika mwenendo wa kesi hatua ambayo inasababisha wananchi kukata tamaa hasa wanapohisi kunyimwa haki zao.

Bwana Shija amebainisha kuwa, wananchi wengi wanapoteza haki zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mashauri mengi kutofikia mwisho, kesi kutomalizika kwa wakati, mchakato wa upelelezi wa kesi na kuandaa mashtaka kuchukua muda mrefu, viashiria vya rushwa kwa baadhi ya watendaji wa vyombo vinavyoshughulika na masuala ya haki, wananchi kushindwa kumudu gharama za uendeshaji wa kesi pamoja na kukosa msaada wa kisheria.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wadau kujadili namna ya kuondokana na changamoto hizo na hasa zisizokuwa za kimfumo ambazo ziko ndani ya uwezo wao, ili kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati.

Wakitoa maoni yao, baadhi ya wadau wameliomba Jeshi la polisi kupitia kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Shinaynga Biasa Chitanda kufuatilia kwa kina kesi zinazofunguliwa katika vituo vya polisi ili zisidhoofishwe na maafisa wasio waaminifu au kuishia njiani, ambapo katika upande wa Mahakama wameshauri uongozi wa juu wa Mahakama kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi zinazofikishwa katika chombo hicho ili kuhakikisha zinatolewa maamuzi kwa wakati na kwa kuzingatia misingi ya haki.

Kufuatia majadiliano hayo Mkuu wa Mashtaka wa mkoa wa Shinyanga Bi. Ajuaye Bilishanga na Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Shinyanga Biasa Chitanda licha ya kuahidi kufuatilia kwa kina kesi zote zinazofikishwa kwenye vituo vya Polisi, wamesema kesi nyingi zinaishia njiani au kukosa nguvu ya kisheria zinapofikishwa pindi zinapofikishwa Mahakamani kutokana na watu wanaotakiwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani ikiwemo waathirika wenyewe kutotoa ushirikiano.

Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro, amesema suala la mwenendo wa kesi na upatikanaji wa Haki linahitaji uaminifu na ushirikiano mkubwa kati ya wadau wote ikiwemo watendewa wenyewe, ili kuepuka kuwapa fursa watendaji baadhi ya watendaji wa Mahakama wasio waaminifu, ikiwemo kuhakikisha ushahidi unaofikishwa mahakamani unajitosheleza.  

Awali akifungua kikao hicho, Afisa Tarafa ya Samuye Bw. Aaron Laizer ambaye alikuwa amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, aliwataka wadau kujadili kwa uhuru ili kupata suluhuhisho la changamoto zilizopo katika upatikanaji wa haki katika Mashauri ya jinai, kwa kuwa haki ndiyo msingi wa Amani na ustawi wa jamii.  

Kikao hicho kimeunda Kamati maalum inayowashirikisha wadu mbalimbali, ikiwemo Mahakama, Jeshi la polisi na Ofisi ya taifa ya Mashtaka, ambao watakuwa na jukumu la kushughulikia changamoto zote zinazojitokeza kwenye mchakato wa upatikanaji wa Haki jinai.

Kaimu Mkurugenzi wa PACESH Bw. John Shija akitoa taarifa fupi ya Mradi wa Mwanamke Salama na mambo ambayo yanapaswa kujadiliwa na wadau

Mjumbe wa Bodi ya PACESH Dkt. Agatha Mgogo ambaye pia ni Mkurugenzi wa chuo Kikuu huria tawi la Shinyanga akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa na kumkaribisha mgeni rasmi.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika kikao hicho Bw. Aaron Loishiye Laizer akifungua kikao kwa niaba ya Mkuu wa wilaya

Bw. Laizer akiendelea kufuatilia mijadala mbalimbali kwenye Kikao

Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Shinyanga Bi. Ajuaye Bilishanga akiwa kwenye kikao cha wadau

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro akiwa kwenye kikao cha wadau

Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi (OCID)Wilaya ya Shinyanga Biasa Chitanda akiwa kwenye Kikao cha wadau

Mratibu wa Mpango wa taifa wa kutokomeza Ukatili kwa wanawake na watoto wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Aisha Omari akiwa kwenye Kikao cha wadau

Wadau wa Haki jinai wakiwa kwenye Kikao

Wadau wakiwa kwenye Kikao

Wadau

Meza kuu

Wadau

Wadau wakitoa michango mbalimbali ya Mawazo namna ya kutatua changamoto zilizopo katika upatikanaji wa Haki jinai (Simeo Makoba Meneja Vipindi Redio Faraja)

Afisa Mradi kutoka wa Mfuko wa ruzuku kwa wanawake Tanzania (WFT-T) Mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akitoa maoni yake

Wadau wakiendelea kutoa maoni yao

Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Shinyanga Bi. Ajuaye Bilishanga akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kwa wadau.

Wadau wakiendelea kufuatilia kikao

Picha ya pamoja kati ya Mgeni rasmi, Mjumbe wa Bodi ya PACESH Dkt. Agatha Mgogo na Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Shinyanga Bi. Ajuaye Bilishanga

Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi na Kamati ya Haki jinai Wilaya ya Shinyanga, mwenye sare ya Magereza ni Afisa sheria wa Magereza Shinyanga Lusaka Clement Shigumha

Picha ya pamoja na wataalam wa Idara za Maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii na afya kutoka Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa kisheria ikiwemo watumishi wa PACESH

Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wadau wa Haki jinai kutoka taasisi zisizokuwa za Kiserikali

Post a Comment

0 Comments