Na Lucas Raphael,Tabora
Mahakama ya Hakimu mkazi wa wilaya ya kaliua mkoani Tabora Imewahukumu kifungo cha miaka 3 mtendaji wa kijiji na mtendaji wa kata baada ya kupatikana ana hatia ya Kuomba na kupokea hongo ya shilingi milioni . 3,000,000.
Akitoa hukumu hiyo leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Felix Ginene alisema kwamba anatoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ovu ambapo kila moja hatatumikia kifungo cha miaka mitatu jela .
Alisema kwamba ili jamii iwe na amani lazima vitendo vya Rushwa vikomeshwe kila sekta na kuacha kutumia madaraka vibaya kwa kujipatia fedha kwa njia zisizokuwa za kiungwana.
Hakimu Felix aliendelea kusema kitendo cha maafisa wa serikali kutumia makosa ya watu wengine kujipatia fedha sio sawa hivyo ni muhimu jamii kuwafishuwa .
Hata hivyo mahakama hiyo imewaamuru washitakiwa hao kumrejeshea Ndilana Budeba kiasi cha shilingi 2,300,000/= ikiwa ni sehemu ya fedha iliyobaki baada kumrejeshea kiasi cha shilingi milioni 700,000/ wakati uchunguzi wa kesi ulipokuwa unaendelea.
Awali mbele ya mahakama hiyo mwendesha Mashtaka wa Serikali David Bakari pamoja na Kajivo Aidan waliiambia mahakama hiyo kwamba Kwamba mnamo tarehe 21/04/2023 watuhumiwa Richard Mpagama Mtendaji wa Kijiji Cha Imagi kata ya Nh'wande na Laurent Isaya Sendu Mtendaji wa Kata ya Nh'wande Wilayani Kaliua Mkoani Tabora waliomba rushwa shilingi milioni 3,000,000
Alisema kwamba waliomba rushwa hiyo kutoka kwa mwananchi mkazi wa kijiji cha Imagi, Kata ya Nh'wande Wilayani , Ndilana Budeba Ili wamwachie huru na aishi kwa amani katika Kijiji hicho Kwa kosa alilounganishwa lililomhusu mkwe wake (mume wa binti yake) kuhusika na wizi wa kutumia silaha.
David Bakari pamoja na Kajivo Aidan waliendelea kuambia mahakama hiyo kwamba kesi ya jinai Na.71/2023 Jamhuri dhidi ya Richard Mpagama na Laurent Sendu kwa kuwatia hatiani kwa kosa la Kuomba na kupokea hongo ya Tsh. 3,000,000/= kifungu kidogo cha 15(1)(a)na (2) cha PCCA (Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022).
Watuhumiwa wametiwa hatiani kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni . 1,000,000/= kila mmoja Washtakiwa wameshindwa kulipa faini na hivyo wamepelekwa gerezani.