Shirikisho
la vyama vya wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Shinyanga nimeiomba serikali
kushughulikia changamoto za wafanyakazi kazi ikiwemo ucheleweshwaji wa mafao
kwa wastaafu, kikokotoo pamoja na nyongeza ya mishahara.
Hayo
yamebainishwa leo na mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Ramadhan Pangara
wakati akisoma risala ya wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi ambazo kimkoa
zimefanyika Kakola Wilaya ya Kahama.
Mratibu
huyo ametaja changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi huku akiiomba
serikali kushughulikia haraka.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Mathias Balele amesisitiza suala la kikokotoo kushughulikiwa
haraka ili kumaliza kero zilizopo.
mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha
ameahidi kuzichujua changamoto za wafanyakazi nakuzifikisha sehemu huzika Ili
ziweze kushughulikiwa.
TAZAMA PICHA ZOTE