SHIRIKA LA TUMAINI KWA WATOTO LAENDELEA KUTOA TUMAINI KWA SHULE WILAYANI NZEGA.

Na Lucas Raphael,Tabora.           

Katika Kuunga mkono jitiada za serikali ,Shirika la Tumaini kwa watoto katika wilaya ya nzega mkoani Tabora limetekeleza miradi ya uboreshaji wa miundombinu ya shule mbalimbali ikiwemo madarasa, visima ,matundu ya vyoo na majiko banifu vikigharimu kiasi cha shilingi milioni 340,500,000/.

Kutoa msaada huo kwa shule za wilaya ya nzega ni kuunga mkono jitiada zinazofanywa ya serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suhulu Hassani ya kuboresha miundombinu ya shule zilipo pembezoni mwa wilaya hiyo hasa vijijini.

Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa shirika hilo Cornelius Maganga mbele ya wajumbe wa  baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya nzega liliofanyika  kwenye kijiji cha Lubisu kata ya Utwigu  wilayani nzega mkoani hapa .

Alisema kwamba wamejenga madarasa 11 katika shule za Mwaguguli shule ya msingi ,Kanolo shule ya msingi,  shule ya msingi Sumbu,na Ibushi shule ya msingi.

Alifafanua kwamba lengo la kujenga madarasa hayo ni  kuisadia serikali  kuboresha miundombinu ya shule hizo kwani walijenga madarasa ya Elimu ya awamu  kisha madarasa ya shule ya  msingi ambayo yanatumika kwa wanafunzi .

Aidha alisema pia walijenga matundu ya vyoo  72 katika shule za Iditima,Mwakipanda,Ibushi,Isanga ,Kabale na Mwakashanhala

Maganga aliendelea kusema kwamba shirika pia lilichimba visima virefu vya maji vipatavyo 6 katika vijiiji vya Kidete ,Kahama Nhalanga,Luhumbo.Nhabala,Kagando na Mwaguguli.

Alisistiza licha maji hayo kutumika kwa ajili ya shughuli za shule pia wananchi wanaozunguka maeneo hayo wanayatumia maji hayo kwa shughuli za kila siku za maisha yao lengo likiwa ni jamii kupata maji safi na salama

Mwenyikiti huyo aliendelea kuwaeleza madiwani hao kwamba licha hayo pia walitengeneza majiko banifu kwa ajili ya kupikia kwenye maeneo ya  shule ili watoto wanaosoma katika shule hizo waweze kupikiwa  chakula muda wa  mchana na kusoma kwa umakini na kuongeza ufaulu .

Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya  nzega, Henerico Kanoga alilishukuru shirika hilo kwa kuweza kujitokeza na kusaidia wananchi wa wilaya ya nzega hasa kwa upande sekta ya elimu.

Alisema kwamba kutolewa kwa misaada hiyo kutachochea ukuaji wa sekta ya elimu katika wilaya hiyo ikiwemo kata na vijiji vya wilaya hiyo .

Hata hivyo aliwataka madiwani kuunga mkono jitiada zinazofanywa na sekta binafsi kwa ajili ya kusukuma  maendeleo kwenye vijijini na kata zetu.

“Madiwani ni muhimu sana kuyasemea mazuri yanayofanywa na shirika la Tumaini kwa watoto na kuwasitizia wazazi na walezi kuhakikisha miudombinu hizo zinatuzwa na kutumika kwa muda mrefu ili kuendelea kuwavutia asasi zingine ziwekeze kwenye Elimu wilayani humo”alisema Henerico

mwisho 

5.  Hicho Ni Kisima Cha Maji  kilichopo katika jijiji cha upina kinachutumiwa kati ya jamii na wanafunzi wanaosoma karinbu na kisima hicho.

 

Previous Post Next Post