TASAC YAANDAA HATI YA MAKUBALIANO NA TTCL PAMOJA USCSAF KWAAJILI YA UJENZI WA MINARA MITATU






Na Gideon Gregory, Dodoma.

Katika kuimarisha mawasiliano katika Ziwa Victoria, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeandaa hati ya makubaliano baina yake na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa ajili ya ujenzi wa minara mitatu
(3) ya mawasiliano ya simu.

Hayo yameelezwa leo Mei 06,2024 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameongeza kuwa Minara hiyo inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa mawasiliano ya simu na vyombo vya usafiri majini katika Ziwa Victoria.

Aidha, amesema ufungaji wa mfumo wa upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa katika
Ziwa Victoria (weather buoy forecast system) unaendelea ambapo vifaa vya mfumo huo vimewasili nchini na kazi za mradi zinaendelea.

“Serikali kupitia TASACimeendelea kusimamia ulinzi na usalama wa vyombo vya usafiri majini katika eneo la Tanzania Bara, udhibiti wa huduma za bandari na watoa huduma za usafirishaji, kutoa huduma ya biashara ya meli kwa bidhaa mahsusi, na kudhibiti uchafuzi wa mazingira
unaotokana na shughuli za usafiri majini.

Ameongeza kuwa kuhusu usimamizi wa watoa huduma zinazodhibitiwa, Serikali kupitia TASAC imeendelea kutoa leseni/vyeti vya usajili kwa watoa huduma waliokidhi vigezo vya kutoa huduma zinazodhibitiwa na kusimamia utekelezaji wa masharti ya leseni hizo kwa mujibu wa sheria na kanuni ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora.

“Hadi kufikia Machi, 2024 jumla ya watoa huduma 1,722 zinazodhibitiwa walisajiliwa na kupewa leseni ikilinganishwa na jumla ya watoa huduma 1,498 zinazodhibitiwa waliosajiliwa na kupewa leseni katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la 14.95%.

Pia amesena TASAC ilifanya ufuatiliaji kwa watoa huduma hao, ambapo, uzingatiwaji wa viwango vya utendaji vya watoa huduma kulingana na kanuni za utoaji wa huduma hizo ulifikia 90.50% ikilinganishwa na asilimia 89 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema fanisi huo ulifikiwa kutokana na juhudi zinazofanyika na Serikali kupitia TASAC
zikiwemo za kufanya ufuatiliaji na tathmini mara kwa mara.
Previous Post Next Post