TIMU 22 ZA MPIRA WA MIGUU KUWANIA UBINGWA SALOME MAKAMBA CUP



Timu 22 za Mpira wa Miguu kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga, zinashiriki mchezo wa kuwania ubingwa kupitia ligi ya Salome Makamba Cup, ambayo inaendelea kurindima katika viwanja tofautitofauti, kwa udhamani wa Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Katibu wa Mbunge Makamba Bw. Justine Mboya, Timu mshindi wa kwanza itajinyakulia zawadi ya Ng’ombe (Mnyama) mmoja, Mshindi wa pili itajinyakulia mbuzi wawili, Mshindi wa tatu itaondoka na zawadi ya Mbuzi mmoja ambapo katika upande wa Mfungaji bora na Mchezaji bora watajinyakulia zawadi ya fedha taslimu.

Washindi watakaopatikana katika mashindano hayo ambayo yamelenga kukuza soka na kuibua vipaji kwa vijana, watakabidhiwa zawadi zao na Mbunge Makamba siku ya Jumamosi tarehe 01.06.2024 baada ya mchezo wa finali utakaochezwa katika uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga.

Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni zile zilizoshinda zawadi ya Jezi na Mpira wa miguu kupitia Programu ya Chemsha bongo na Salome Makamba inayoendeshwa na Redio Faraja kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga Salome Makamba, ambazo ni Mitumbani FC, Ngokolo Stars, Mwadui United FC, Mwagala FC, Mwamagunguli FC, Mchicha FC, Kabondo FC, Bugweto FC, Mwalugoye FC, Chipukizi FC, Ndala FC na Msituni FC.

Nyingine ni Home boys FC, Katunda FC, Mbezi City FC, Ngalya FC, Boko FC, Magereza FC, Mshikamano FC, Town Stars FC, Shinyanga Veteran FC na Chita FC.
Previous Post Next Post