Pumu ni ugonjwa
unaoathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu
yanazojulikana kitaalamu kama bronchioles.
Mtu
mwenye pumu husababisha kuvimba kwa kuta za mirija, kujaa kwa ute mzito na
kupungua kwa njia ya kupitishia hewa.
Hali hiyo humsababishia mwathirika kushindwa kuvuta na
kutoa hewa nje, hivyo kupumua kwa shida.
Pia,
hali hiyo inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili
kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.
Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha
yake.
Pumu husababisha na nini?
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa
pumu, ikiwamo matatizo ya kinasaba.
Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia
unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.
Magonjwa ya mapafu kama bronchitis Vyanzo vya mzio
(allergens) kama vumbi, kinyesi cha wanyama na baadhi ya vyakula.
Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu
kali.
Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye
viwanda vya rangi, chuma, saruji na vigae.
Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na
baadhi ya virusi na bakteria kama pneumonia.
Tiba
Tiba mbadala inaweza kuondoa tatizo la pumu kwa
mgonjwa.
Chukua magome ya mizizi ya mlimao kiasi (kama mkono
mmoja), chemsha kwenye maji lita moja kisha maji yake tia tangawizi ilosagwa
nusu kikombe na asali nusu lita, chemsha kunywa kikombe kimoja mara tatu.
Au:-
Chukua majani ya ngogwe na majani ya tura chemsha
pamoja na kidonge kimoja cha halititi, kisha kunywa glasi moja kutwa mara tatu
ikiwa vuguvugu, unaweza iunga na sukari ili ilete ladha nzuri
Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu wa tiba mbadala