WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA SHINYANGA WAMEIPONGEZA NA KUISHUKURU EWURA KANDA YA MAGHARIBI KWA KUHITIMISHA MAFUNZO KASHWASA KWA VITENDO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi kwa kuhitimisha mafunzo yao kwa vitendo.

EWURA kanda ya Magharibi ilianza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga siku ya jana ambapo leo Ijumaa Aprili 3,2024 imehitimisha mafunzo yake kwa kufanya ziara ya kutembelea na kufahamu mambo mbalimbali, katika mradi mkubwa  wa kusambaza majisafi kutoka Ziwa victoria hadi miji ya Kahama na Shinyanga (KASHWASA)  uliopo Ihelele Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

Waandishi wa Habari waliotembelea katika mradi huo wameipongeza na kuishukuru EWURA kwa ubunifu huo ambao umelenga kuwaimarisha katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wakati wa kuripoti habari za Nishati na Maji.

Wameahidi kutumia vema kalamu zao katika kuhabarisha wananchi huku wakiziomba mamlaka zingine kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze kuendelea kuripoti habari zao kwa weledi kwa lengo la kutengeneza taifa bora.

Akizungumza meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher  amewasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuripoti habari zenye uhalisia ili wananchi wapate ueleza zaidi kuhusiana na upatikanaji wa maji na matumizi yake.

Mhandisi Christopher pamoja na mambo mengine ameelezea umuhimu wa ziara hiyo kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema EWURA kanda ya Magharibi itaendelea kushirikiana na waandishi wa habari kutoka Shinyanga Press Club (SPC).

“Tumefanya haya mafunzo kuanzia jana leo tumefanya ziara kwahiyo mafunzo haya ni muunganiko wa mafunzo ambayo tulianza kuyafanya jana ambayo tulielezana kinagaubaga kazi ambazo EWURA inafanya majukumu ambayo EWURA inafanya na tuliona katika sekta hizi mbali ambazo tunazidhibiti za Nishaji na Maji na tuliona kwenye sekta ya maji mamlaka ambazo tunazidhibiti ziko mamlaka 12 kama tulivyoelezana jana moja wapo ni mamlaka ya Maji KASHWASA”.

“Tuliona ni vizuri kutembelea mradi wa maji KASHWASA kwa sababu unavitu vingi kwanza maji yenyewe yanatoka ziwani na ziwa Victoria ni ziwa kubwa na maji yanaenda kwenye Mikoa mingi kwahiyo tukaona wakija hapa watajifunza mambo mengi ambayo yanahusiana na kazi ambazo tunazifanya sisi kama EWURA kwahiyo nashukuru sana kwa kutupokea ninaimani kwa waandishi wa habari hasa wanachama wa Shinyanga Press Club mmejifunza mambo mengi ambayo yanahusiana na shughuli za usambazaji wa huduma za Maji, na tunaimani baada ya kutoka hapa mtakuwa mnatoa habari ambazo nizauhakika zinauhalisia katika jamii”. Amesema Mhandisi Christopher

Kwa upande wake meneja huduma kwa wateja  KASHWASA John Ngano ameeleza kuwa mradi huo ulipangwa kuzalisha Lita za ujazo milioni 80 kwa siku lakini mpaka sasa wanazalisha milioni 67 na kuwauzia mamlaka za maji na jumuiya ndogo ndogo za watumia maji.Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher akizungumzaMeneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher akizungumza

Meneja huduma kwa wateja  KASHWASA John Ngano akizungumza.

Mkuu wa kituo cha uzalishaji Maji KASHWASA Mhandisi Cheyo Kanunda akizungumza.

 

Previous Post Next Post