Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI MANISPAA YA SHINYANGA WASHAURI KUBORESHWA VYANZO VYA MAPATO YA NDANI, MEYA MASUMBUKO ATAJA JITIHADA ZILIZOPO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wameiomba Halmashauri hiyo kuendelea kubuni zaidi vyanzo vya mapato na kuviboresha vilivyopo ili kukuza Uchumi, ustawi na Maendeleo  ya Halmashauri, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Wakizungumza na Misalaba Media  kwa nyakati tofauti wananchi hao wamependekeza kuboreshwa kwa vyanzo vya mapato ya ndani vilivyopo ikiwemo masoko, stendi za mabasi, miundombinu ya barabara na kuongeza viwanda.

Kwa upande wake Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema Halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi la ukusanyaji wa mapato linafanikiwa huku akiwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi hilo.

Ametaja hatua mbalimbali za mafanikio katika zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutoka Mwaka wa fedha 2019\2020 hadi Mwaka wa fedha huu 2023\2024.

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakati sisi tunaingia kwenye Halmashauri hii baada ya kupata uwakilishi kwa maana ya kuwa madiwani wa kata tulikuta bajeti iliyotengwa na Halmashauri Mwaka wa fedha 2019\2020 ilikuwa ni bilioni tatu na 23 elfu 228 na 546 ambayo ndiyo makusanyo yaliyotarajiwa kukusanywa kwa ajili ya Mwaka huo wa fedha lakini Halmashauri kwa wakati huo iliweza kukusanya bilioni mbili 375 milioni na 70 elfu na 340 ambayo ni sawa na asilimia 79 lakini sisi tukaboresha tukasema hapana vyanzo vya mapato havijakaa vizuri kwahiyo tukatengeneza bajeti tukataka makusanyo yetu yawe bilioni nne na 11 elfu 648 na 719 na senti hamsini lakini tuliweza kukusanya bilioni tatu na 316 na 879 na 585. 79 ambayo ni sawa na asilimia 83 sasa hapa kulitokana na changamoto ambazo ilikuwa ni pamoja na marekebisho ya hile vyanzo ambavyo tulidhani vimeachwa au kuwekewa mkazo katika kukusanya”. Mhe. Masumbuko

“Mwaka wa fedha 2021\2022 tukaimarisha maeneo yetu ya vyanzo bajeti yetu tukaipandisha ikiwa ni bilioni nne na 11 milioni 648 na mia nane, katika Mwaka huo tukasimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa matumizi tulifanikiwa kukusanya bilioni tano na milioni 62 na 92 elfu na 290 ambayo ni sawa na asilimia 125”.

“Sasa vile vyanzo ambavyo tuliweza kuviimarisha tukaviwekea nguvu zaidi hatukuongeza kodi hatukubadilisha aina ya vyanzo ikabaki ni palepale tukatengeneza mikakati ya namna bora ya ukusanyaji tukaunda kamati ambazo ziliwahusisha watu wanje wakiwemo wafanyabiashara maarufu wafanyabiashara wadogo na wa kati tukahusisha viongozi wa dini tukahusisha kamati ya usalama ya Wilaya na watu wengine tukatengeneza kamati maalum ambayo itasimamia na kuratibu namna bora ya ukusanyaji wa mapato kwahiyo bajeti yetu tukaitengeneza ikiwa ni bilioni tano na 711 elfu, milioni 618 na 25 lakini tukafanikiwa kukusanya bilioni sita na milioni 149  na 239 elfu na 579 sawa na asilimia 108 hiyo ni Mwaka wa fedha 2022\2023”.

“Sasa huu Mwaka wa fedha 2023\2024 Halmashauri yetu imekusudia kukusanya bilioni sita lakini mpaka sasa tumeshafanya makusanyo zaidi ya asilimia 76 uzuri sisi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tumekuwa tukiwashirikisha sana wananchi ambao wanatoa huduma mbalimbali namna ambavyo wanapaswa kulipa kodi za serikali hii inaturahisishia sana lakini pia sisi kamati ya ufuatiliaji tumeijengea nidhamu namna bora ya kuweza kufuatilia kodi zetu ambazo ndizo zinawezesha Manispaa kufanya miundombinu mbalimbali ya uboreshaji na ustawi wa wananchi wetu wa Manispaa ya Shinyanga wito wangu kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wawe tayari kutuunga mkono lakini zaidi kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan”.amesema Mhe. Masumbuko

Wakati huo huo wananchi hao wameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuendelea kuhamasisha wananachi kushiriki vyema katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

TAZAMA VIDEO WANANCHI WAKIONGEA

 


 

Post a Comment

0 Comments