WANANCHI WA HALMASHAURI YA MPIMBWE WILAYANI MLELE MKOANI KATAVI WAPONGEZA MABORESHO YA HUDUMA ZA AFYA KWA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

Wananchi wa Vijiji vya Ilalanguru na Minyoso katika Halimashauri ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa Kuboresha Miundombinu  ya afya pamoja na Kuongeza huduma mbalimbali za kiafya ikiwemo huduma ya meno,macho,upasuaji na huduma ya mama na mtoto ambazo zilikua azipatikani katika Hospitali ya Wilaya hiyo na Kuondoa adha kubwa ya kufuata huduma hizo katika mikoa jirani.

 


Wakizungumza Kwa nyakati tofauti tofauti Wananchi hao wamesema kutokuwepo Kwa huduma hizo walilazimika kutumia gharama kubwa kuzifuata ila Kwa sasa wanamshukuru dkt.samia kwa Kuendelea Kuboresha Sekta ya Afya katika Halimashauri yao.

 


Mganga Mfawidhi wa hospital ya Wilaya ya Mpimpwe Dr.Urio Musa Ferdinand amesema, Wananchi walikuwa wakilazimika kufuata baadhi ya huduma za kiafya ikiwemo huduma za kiuchunguzi kama vile exlay na ultrasound katika Mkoa wa rukwa.

 

Akielezea mafanikio ya Miaka 3 ya dkt.samia Suluhu Hassan katika Halimashauri ya Mpimpwe katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya Kaimu Mkurugenzi wa Halimashauri  Mwl.charles Ferdinand amesema.

 

Hospitali ya halimashauri ya Mpimpwe inahudumia zaidi ya Wananchi laki mbili wa vijiji 31 kutoka katika kata 9 za Halimashauri ya Mpimbwe.

Previous Post Next Post