WATU 11 WAFARIKI DUNIA KWA HITILAFU YA UMEME KIWANDANI

Picha hii ya mtandaoni haina uhusiano na tukio la kiwanda Cha mtibwa 


WATU 11 wafanyakazi wa kiwanda Cha Sukari Cha Mtibwa mkoani Morogoro wamefariki Dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia Hitilafu  ya umeme Kiwandani hapo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama ameibia Matukio Daima media kuwa ajali hiyo  imetokea majira ya saa saba na nusu, usiku wa kuamkia leo.

SACP Mkama amesema chanzo  cha ajali hiyo ni baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye mtambo wa kupitisha mvuke wa kuzalisha umeme kiwandani hapo.

Picha ya tukio la kiwanda Cha Sukari Mtibwa


Kamanda huyo wa Polisi akasema waliofariki dunia ni pamoja na raia wa kigeni wa nchi tatu tofauti na ambao ni wataalamu wa umeme na mitambo waliokuwa kwenye chumba cha kuendesha mitambo hiyo.


Aidha majeruhi watatu wa ajali hiyo wamepelekwa hospitali ya Misheni ya Bwagala kwaajili ya matibabu zaidi.

Previous Post Next Post