Na Mapuli Kitina Misalaba
Wazazi, walezi na jamii wameshauriwa
kuendelea kuwalea watoto katika misingi ya mila na desturi ili kuimarisha
utamaduni wa kila kabila na kuepukana na mmomonyoko wa maadili hapa nchini.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wazee
wakazi wa Himaya ya Busiya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani
Shinyanga, wakati wakizungumza na Misalaba Media.
Wamesema mmomonyoko wa maadili hasa kwa
vijana unatokana na malezi mabaya yanayoanzia ngazi ya familia na jamii kwa
ujumla ambapo wamesema ni vema wazazi kuwafundisha watoto mila na desturi za
kabila husika ili kuwaepusha na tabia za kuiga mila za kigeni.
Pia wameishauri serikali nchini kuwapa
kipaumbele wazee na viongozi wa kimila katika hatua za kutokomeza mmomonyoko wa
maadili.
Wamesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi
kikuwa ikiwemo vijana kuwaepusha na makundi mabaya yanayopelekea mmomonyoko wa
maadili, vitendo vya ukatili na ndoa za utotoni.