WIMBI LA WANUNUZI WA MPUNGA LATAJWA KUWANYONYA WAKULIMA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA ATOA MAELEKEZO

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga nimemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wataalam wake kufuatilia na kuwasimamia wakulima katika hatua zote za kuuza mazao yao ili waweze kunufaika.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje baada ya Diwani wa kata ya Lyamidati Mhe. Veronica Nduta kuwasilisha taarifa na changamoto za kata hiyo.

Diwani huyo amesema ipo changamoto ya wafanyabiashara wanaonunua zao la Mpunga kwa wakulima kutumia vipimo vikubwa hali ambayo inakosesha faida kwa wakulima.

“Kata ya Lyamidati ni kata ya wakulima wa zao la Mpunga na kwa Mwaka huu Mungu kajalia kata ile imapata Mpunga kwa wingi ila sasa kuna wimbi limejitokeza la wanunuzi wa Mpunga wanatumia yale Madum makubwa yanayowanyonya wakulima naomba serikali iangalie hili ili kuweza kuwasaidia wakulima hawa wawe na faida na mazao yao”.amesema Mhe. Veronica

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amemsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufuatilia changamoto hiyo ili wakulima waweze kuuza zao la Mpunga kwa tija.

“Sisi kama Halmashauri tuna sheria ndogo lakini vinagusa kwenye vipimo kwamba ni kiasi gani Gunia linatakiwa liwe na ujazo sasa kama kuna shida hiyo sisi kama Halmashauri tunatakiwa twende tukahakikishe kwamba mkulima wetu hapunjwi mkurugenzi na timu yako fuatilieni hili unakuta sahzi kuna watu wanapima lita kumi kumi mbili wanazifanya kuwa debe moja mana nake anapima lita kumi 12 ndiyo anapata debe 6 halafu anasema amepima gunia sasa hapo mkulima anaenda kujikwamua kiuchumi maana yake Mpunga wake utaisha bila kuwa na kipato kwahiyo tuombe tu mkurugenzi na timu yako uhakikishe kwamba unalifuatilia hili ili liweze kuisha tufuate zile taratibu tulizoziweka lakini upande wa katibu tawala wa Wilaya naye atafuatilia kwa sababu naye anaye wakala wa vipimo aangalie Dumbesa zisiwepo”.amesema Mhe. Mboje

Wakati huo huo Mhe. Ngassa Mboje amewahimiza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuendelea kushirikiana na wataalamu ikiwa ni pamoja na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato ya ndani na kuongeza kasi katika utatuzi wa kero za wananchi.

Amesisitiza kuimarisha ushirikiano kati ya watendaji wa kata na wenyeviti wa kamati ya kata ya maendeleo (WARDS) kwa kuhakikisha taarifa za maendeleo ya kata kila mmoja anafahamu hatua kwa hatua ili kuepusha mkanganyiko.

Pia baraza hilo la madiniwa kupitia mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Ngassa Mboje amemkumbusha mkurugenzi kuwaelekeza watendaji wa vijiji kusoma taarifa za mapato na matumizi katika mikutano ya hadhara ili wananchi waweze kufahamu fedha na hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mei 8,2024 limefanya Mkutano wa kawaida  kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kila kata kwa kipindi Cha robo ya tatu ya Mwaka wa fedha 2023\2024.

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri hiyo katika Mkutano wa kawaida  kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo  kwa kipindi Cha robo ya tatu ya Mwaka wa fedha 2023\2024.

Diwani wa kata ya Lyamidati Mhe. Veronica Mabeja Nduta akizungumza kwenye baraza hilo.






 

Previous Post Next Post